Zinazobamba

MAMA KANUMBA ASIFIA TAMASHA LA KUWAKUMBUKA WASANII WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI

Na Mussa Augustine 

Bi Flora Mutegoa ambaye ni mama yake aliyekua  Muigiza Nguli wa Bongo Movie Marehemu Steven Charles Kanumba amefunguka nakusema kuwa Tamasha la Kuwakumbuka Wasanii Waliotangulia Mbele za Haki linawapa heshima Wasanii hao licha ya kutokuwepo kimwili lakini Kiroho bado wapo hai.

Mama Kanumba amesema hayo mapema leo Septemba 7 wakati akizungumza na Wanahabari,kwenye Tamasha la Kuwakumbuka Wasanii Waliotangulia Mbele za Haki lililofanyika katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es salaam,ambapo tamasha hilo limehudhuliwa na Wasanii mbalimbali pamoja na watu mashuhuri.

Amesema kwamba Tamasha hilo ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza tangu mwanae Kanumba  afariki dunia Mwaka 2012 limekua nila muhimu sana kwani linawaleta pamoja Wasanii ili kuonesha upendo.

" Namshukuru Mungu kwa Kuwapa Maono ya kuandaa tamasha hili kwani ni miaka 12 sasa tangu mwanangu Kanumba afariki Dunia, nikahamia Dar es salaam sikuweza kushuhudia tamasha kama hili" amesema Mama Kanumba.

Nakuongeza kwamba" Namshukuru Mwanangu Steve Nyerere kwa kushirikiana na kamati yake kuandaa Tamasha hili ,amekua na ubunifu mkubwa na Maono ya mbali sana ,tuendelee kushirikiana ili tufanikishe tamasha hili lifanyike Kila Mwaka kwa ufanisi Mkubwa.


Hakuna maoni