Zinazobamba

NIBUSARA KUWAKUMBUKA WASANII WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI: CHUCHU HANSI

Na Mussa Augustine.

Msanii wa Bongo Movie , Chuchu Hansi, amesema  kuwa ni jambo la busura kuwambuka wasanii ambao wametangulia mbele ya haki na kuendeleza mazuri yao. 

Chuchu amesema hayo muda huu katika shughuli ya kuwakumbuka wasanii mbalimbali wakiwemo watangazaji na watozi wa filamu waliofariki dunia ambayo umefanyika jijini Dar es Salaam. 

Msanii huyo pia amefafanua kuwa katika kuenzia mazuri ya wasanii waliofariki dunia, ameshirikisha baadhi ya wasanii waliokwenye kituo cha Sanaa cha Mzee Majuto kilichoko jijini Tanga. 

"Wapo baadhi ya wasanii ambao nimewashirikisha kutoka kwenye kituo cha Mzee Majuto na 'soon' mtaweza kuwaona pindi itakapoanza kuoneshwa katika kituo cha runinga nilipoipeleka, amesema.

Hakuna maoni