MONALISA ATOKWA MACHOZI AKITAMBULISHA WATOTO WA MAUNDA ZORRO
Na Mussa Augustine
Wakati akitambulisha baadhi ya wageni waliohudhuria katika shughuli ya kuwakumbuka na kuwasomea dua Wasanii ambao wametangulia mbele ya haki, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Ivone Shell ( MONALISA) Machozi yamembubujika baada ya kutaja Majina ya watoto wa Maunda Zorro.
Aidha Tamasha la Faraja Kwa Wasanii na kuwaombea dua wasanii zaidi ya 250 ambao wametangulia mbele ya haki kwa miaka tofauti limefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club
"Nawaona watoto wa rafiki, ndugu yangu, Maunda Zorro ( Choziii), Mungu awabariki sana na jambo hili litaendelea, huu ni mwanzo, hadi Sasa idadi ya wasanii wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki ni zaidi ya 250 na tutaendelea kuondoka na hatujui nani baada ya hapa ataanza , amesema Monalisa huku Machozi yakimtoka kwa Uchungu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni