Zinazobamba

RAIS DKT SAMIA APONGEZWA KWA KULETA UNAFUU KWA WAMACHINGA.


Na Mussa Augustine.

Umoja wa Machinga Mkoani Kagera imeishukuru serikali kwa Kuwapatia Fedha ya Kununua eneo la Kujenga Ofisi ya Wamachinga Mkoani humo.

Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Septemba 11,2024  Katibu wa Maboresho ya Katiba ya Taifa ya Machinga ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Machinga Mkoa wa Kagera Bi Husna Mohamed Abdalah amesema kuwa kwa kipindi cha uongozi  Rais Dkt.Samai Suluhu Hassan imesaidia kuwaunganisja Wamachinga na Serikali ambapo kundi hilo kwa sasa limekua likishirikishwa kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.

"Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa Kulithamini kundi hili( Wamachinga) nakutupa bure kiwanja chenye thamani ya shilingi milioni  ishirini na saba,pamoja na kutupatia Fedha taslimu kiasi cha  shilingi milioni Kumi za ujenzi wa Ofisi ya Wamachinga Mkoa wa Kagera.

Aidha Katibu Husna amesema kwamba amekua akizunguka Wialaya zote Mkoani huo kwa ajili ya kubaini na kutatua changamoto zinazowakumba Wamachinga ili waweze kufanya biashara zao katika Mazingira mazuri.Wakati huo huo Katibu Shirikisho la  Machinga Mkoani Kigoma Amry Athuman ameishukuru Serikali kwa kuweza kufungua fursa za uwekezaji Mkoani humo kwani umekua chachu ya Maendeleo.

" Nashukuru serikali kwa kufanya Kongamano kwa ajili ya Uzinduzi wa Kiwanda Cha Mabati na Saruji ,hatua hiyo nilikua sijaiona miaka yote niloyoweza kuishi Mkoani Kigoma" amaema

Aidha Athumani amesema kuwa Wamachinga wanakilio kikubwa Cha ukosefu wa Soko ambapo Leo hali hiyo imewakosesha fursa,nakumuomba Rais Dkt Samia kuwajengea soko la Kisasa.

" Hali ya kukosa soko inasababisha tukose Mikopo kwenye taasisi za kifedha kwasababu hatuaminiwi, sisi tunaomba soko tu tujengewe amesama Athumani.

Aidha Katibu huyo ameahidi Kushirikian na Wamachinga Mkoani humo kutatua changamoto zinazowakabili ili kufikia Malengo yao.

Hakuna maoni