Zinazobamba

MASAMAKI AIOMBA SERIKALI KUWAPATIA ENEO LA KUDUMU LA KUFANYIA BIASHARA.

Salum Masamaki


Na Mussa Augustine 

Mwenyekiti wa Chama Cha Machinga Mkoa wa Ruvuma Salum Masamaki ameiomba Serikali kuwapatia eneo la Kudumu la kufanyia Biashara kwani eneo walilopewa kwa sasa nilakupangisha kwa muda.

Ombi hilo amelitoa leo Septemba 11,2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa eneo lililopo Mtaa wa Majengo Mpya wamekua wakipewa Mkataba wa Mwaka mmoja mmoja na hawarusiwi kujenga vizimba vya Kudumu hivyo hali hiyo inawasababishia hali ya kutokuaminika kwenye taasisi za kifedha kupata Mikopo.

" Tunachangamoto kubwa ya kukosa eneo la Kudumu la kufanyia Biashara,eneo tulilopewa haturuhusiwi kujenga vizimba vya Kudumu,naomba serikali kwa niaba ya Wamachinga wote mkoa wa Ruvuma tupewe eneo la Kudumu la kufanyia Biashara,," amesisitiza Masamaki.

Nakuongeza kuwa kwasasa baadhi ya Machinga wamekua wakipanga bidhaa pembezoni mwa barabara kutokana na kukosa Maeneo ya kufanyia Biashara hivyo serikali inapaswa kuangali suala hilo kwa jicho la kipekee ili kuwanusuru na Changamoto zinaaowakumba.

" Naomba tukienda ofisini ya Mkuu wa Mkoa,Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri watupe Ushirikiano" amesema
                      Salum Masamaki
Akizungumzia kuhusu vitambulisho vya Ujasiliamari Masamaki amesema hapo awali  Vitambulisho hivyo viliwasadia kutambulika hata kuweza kupata Mikopo,hivyo ameiomba Serikali iwapatie vitambulisho hivyo kwa awamu nyingine.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ameipongeza serikali ya Dtk Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Ofisi za Machinga Kila Mkoa hali ambayo inawasiaidia kufanya kazi zao kwa kufahamiana kwa ukaribu zaidi na kutatua changamoto zinazowakabili.

Hata hivyo ametoa rai kwa Wafanyabiashara Kuzingatia maagizo yanayotolewa na Viongozi wao ili kuweza kufanya maboresho nakufikia Malengo waliyojiwekea.

Hakuna maoni