Zinazobamba

HALOTEL TANZANIA YATEMBELEA KITUO CHA WATOTO CHA HUMAN DREAMS, KUWAHUDUMIA WATOTO WA KITU HIKO

Dar es Salaam, Tanzania

Leo September 16, 2024 Kampuni ya mawasiliano ya Halotel Tanzania imefanya ziara maalum katika kituo cha watoto cha Human Dreams Children Village kilichopo Kigamboni Jijini Dar es salaam, kituo hicho kinachojihusisha na kulea watoto yatima wenye ulemavu. 

Ziara hii ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kutoa msaada na kusaidia jamii inayohitaji.

Wafanyakazi wa Halotel walifika katika kituo hicho na walitoa msaada wa vifaa mbalimbali, vikiwemo mahitaji muhimu ya kila siku kama vile vyakula, vifaa vya ndani vya kila siku pamoja na fedha. Ziara hii ni sehemu ya mpango wa Halotel kusaidia makundi maalum ndani ya jamii kama sehemu ya uwajibikaji wa kijamii.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Halotel, Bi. Happy Mushi alisema, "Tunatambua changamoto ambazo watoto wenye ulemavu wanazipitia, na ni jukumu letu kama kampuni kuhakikisha kwamba tunawasaidia ili waweze kufikia ndoto zao. Tunatumaini msaada wetu utaleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto hawa."

Viongozi wa kituo cha Human Dreams Children Village walionyesha furaha yao kwa ziara hio, wakisema kwamba msaada wa Halotel utawezesha kuboresha hali ya maisha ya watoto wao. 

Ziara ya Halotel imewapa furaha kubwa na faraja watoto hao, ambao mara nyingi wanahitaji upendo na msaada wa karibu kutoka kwa jamii.

Halotel Tanzania inajivunia kuendelea kushiriki katika miradi ya kijamii, kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma bora za mawasiliano na shughuli za kijamii zinazolenga makundi yenye uhitaji.


Hakuna maoni