Zinazobamba

BANANGA KUWA MGENI RASMI MAHAFALI YA CHUO CHA FURAHIKA.


                       Dkt.David Msuya

Na Mussa Augustine.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 20 ya Chuo Cha Ufundi Stadi, Furahika yatakayofanyika Septemba 28 Mwaka huu jijini humo. 

Taarifa hiyo, imetolewa Septemba 7,2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt David Msuya alipozungumza na waandishi wa habari na kufafanua kwamba katika kipindi hiki ambapo mahafali yanafanyika, dirisha la usahili wa wanafunzi wapya linafunguliwa na kuwaomba wazazi kupeleka vijana wao kwa ajili ya muhula mpya wa masomo.

“Dirisha la usahili tayari limefunguliwa hivyo naomba wanafunzi waje kujisajiri kwa msimu mpya wa Mashimo, na mwisho wa udahili ni Oktoba 30 mwaka huu kwa kozi mbalimbali hivyo ni vizuri wakatumia fursa hiyo mapema kabla ya usahili”, amesema.

Dkt  Msuya ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaunga Mkono,pamoja na chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendelea kuhakikisha watoto waliopo kwenye maeneo yao wanawapeleka chuoni hapo kupata elimu.

Amesema Chuo hicho kinapokea  vijana kuanzia darasa la saba,ambapo imekuwa ni faraja kwao kutokana na zaidi ya asilimia 75 ya vijana wanaohitimu chuoni hapo wanapata ajira kirahisi katika maeneo mbalimbali hususan ya hoteli.

Aidha ameongeza kwamba ili kuendeleza dhamira yao ya kutoa elmu bure kwa wanafunzi wanaokidhi vigezo vya kupata elimu bure, wametia rai kwa wadau wa maendeleo hususan wa elimu kujitokeza katika kutoa misaada ya vifaa vya kufundishia ikiwemo magari.

"Tunaomba watusaidie hata kama magari ni mabovu tutayatengeneza ili tuweze kutoa mafunzo kwa Vijana wanaosoma kozi za udereva hapa chuoni" amesema.

Pia amewakumbusha  wazazi kwamba mwanafunzi wanaojiunga katika chuo hicho ambao  wamo katika mpango wa elimu bure wanalipia kiasi cha  Shilingi 50, 000 kwa ajili ya usajili wa mitihani yao na si vinginevyo, hivyo anawakaribisha kutoka Mikoa mbalimbali hapa Tanzania Bara na Zanzibar kujitokeza kujiunga na chuo hicho ili kupata elimu itakayowakomboa katika maisha yao.

Pia amebainisha kuwa  kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Zanzibar, Septemba 15 mwaka huu wataendesha semina katika kisiwa hicho yenye lengo la kuondoa unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa jamii na kuwahamasisha kujiunga na vyuo vya ufundi ili kutengeneza fikra mpya kwa ajili ya kuwaondoa katika mawazo yasiyo rafiki.

“Tunaamini ukatili unaanzia katika jamii, hususan kwa vijana ambao wanakuwa hawana shughuli za kufanya ambao baadhi yao wanaweza kujiingiza katika makundi hatarishi yakiwemo ya matumizi ya dawa za kulevya, udangaji na kusababisha mimba za utotoni, hivyo tukiwapa elimu ya kupinga ukatili na kuwashawishi kujiunga na vyuo vya ufundi naamini changamoto hiyo itaondoka,” amesema.

Dkt Msuya amefafanua kuwa mchakato wa kutoa elimu hiyo kupinga unyanyasaji unaanzia  katika ngazi ya Shina ambako wanaamini ndiko tatizo linapoanzia, na kuendelea ngazi ya Kata hadi Taifa.

Ameongeza kuwa Mchakato wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa Kijinsia  walianza Tanzania Bara katika Kata ya Mindu, Mkoani Morogoro na Chalinze Mkoani Pwani na sasa wamegeukia Zanzibar na baada ya hapo watakwenda Dodoma.

Hakuna maoni