Zinazobamba

TMA YATABIRI MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI MWEZI OCTOBA_DISEMBA



Na Mussa Augustine 

Mvua za chini ya Wastani wa katika maeneo mengine zinatarajiwa kuanza kwa kusuasua na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usiridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijin Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dkt. Lasislaus Chang'aa amesema mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika ukanda wa ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Octoba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba ,2024.

Dkt Chang'a amesema kuwa Msimu wa mvua  za vuli mahususi itakuwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki ambapo ni mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro, Pwani ya kaskazini, kaskazini ya mkoa wa Morogoro, Mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya mafia), Dar es salaam, Tanga na Mikoa ya ukanda wa ziwa Victoria.

Aidha ameelezea Kanda ya Ziwa Victoria mvua za mvuli zinatarajiwa kuwa wastani Hadi chini ya wastani katika mengi ambapo zitaanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika Mikoa ya Geita, Kagera, na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma na kutawanyika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Octoba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi  Disemba , 2024.

Pia amefafanua kuwepo na mvua ya vuli za wastani maeneo ya Pwani , morogoro, visiwa vya mafia , Dar es salaam, Tanga na visiwa vya unguja na Pemba zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya Tatu ya mwezi Oktoba , 2024 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.

Na nyanda za juu kaskazini Mashariki ambayo ni Mikoa ya Arusha, Manyara, na Kilimanjaro kutakuwa na mvua za wastani hadi wastani kuanza wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2024 na kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.

Hakuna maoni