Zinazobamba

MAADHIMISHO YA WIKI YA AZAKI KUFANYIKA MKOANI ARUSHA.


Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil society(FCS),Justice Rutenge amesema kuwa Maadhimisho ya sita ya Wiki ya Asasi za Kiraia( AZAKI) yatafanyika kuanza  Septemba 9 hadi 13 ,2024  Mkoani Arusha.

Hayo ameyasema leo Agost 23,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea maadhimisho hayo ambayo yana kauli mbiu isemayo Sauti(Voice)Dira ( Vision) na Thamani( Value).

Rutenge amesema kuwa kila mwaka AZAKI inautaratibu wa kuazimisha ikiwa na kauli mbiu mpya ambapo kwa Mwaka huu  inaendana na matukio muhimu ya mwaka ikiwemo kuelekea Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mtaa,pamoja na Uchaguzi Mkuu Mwakani.

"Mwakani tunatarajia kuzindua Dira ya Taifa 2050 ambayo ni fursa inakuja mara moja baada ya miongo mitatu katika kuandaa Dira ya Taifa,tulianza na Dira ya Taifa mwaka 2025, hivyo fursa hii ina umuhimu Kwa sauti za wananchi kusikika, tuondoke kwenye tamaduni ya namna mipango ya Serikali kuandikwa na jopo la wataalamu ambao wanachukua mawazo yao wenyewe na Wanalinganisha na nchi nyingine ndipo wanatengeneza dira ya Taifa bila Kuzingatia Sauti za Wananchi"amesema

Nakusisitiza kuwa "Dira ya Maendeleo ya Taifa inapaswa itokane na Sauti,Mtazamo na Maoni ya wananchi ndiyo maana tunasema sauti ni kipengele muhimu kwenye kaulimbiu ya wiki ya Azaki".

Aidha amesema ifikie wakati Dira yenyewe  iwe na  Makubaliano ya  maoni ya Watanzania kuhusu Dira hiyo inavyotakiwa  kuwa pamoja na kuwepo kwa  tofauti za kidini ,kiumri na kijinsia,ikiwa lengo ni kupata Dira moja tu iliyozingatia Maoni ya Wananchi.

Akizungumzia "Thamani" Rutenge amesema kwamba  jambo hilo limekua likisahaulika mara kwa mara,hivyo ni vizuri kutengeneza mipango mizuri inayozingatia sauti za wananchi ambayo imechukua maoni yao na kuwepo kwa Utekelezaji mzuri wa Maoni hayo.

"Thamani inaamanisha kwamba tunawezaje kutoa Thamani ya maono tuliojiwekea kama Taifa?,Hivyo tunacho sisitiza wiki ya Azaki ni kwamba Thamani tutaipata kwa ushirikiano wa  sekta,nyanja na watu wa aina mbalimbali, kila mtu ashiriki katika mchakato wa maendeleo ya Taifa letu"amesema Rutenge.

Awali Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKI Bi.Nesia Mahenge amesema kuwa imekuwa utamaduni wa Kawaida kukutana  Kila Mwaka kwa lengo la Kujifunza kama Sekta ya Asasi za Kiraia,kuangalia changamoto wanazokutana nazo,na vitu gani wanaweza kuvifanya kwa kushirikiana pamoja.

"Tunaposema Mashirikiano katika Sekta zote tunamaanisha  sekta ya Azaki ambayo ni Asasi za kiraia, upande wa Serikali,Sekta binafsi pamoja  na wadau wa  maendeleo Kwa ujumla namna gani tutashirikiana kuleta maendeleo Nchini Tanzania.

"Watu zaidi ya 500 watahudhuria katika maadhimisho hayo  wakiwemo kutoka  Serikalini,watu binafsi na makundi mbalimbali kutoka sekta za kiraia,ambapo pia kutakua na maonesho mbalimbali" amesema.

Hakuna maoni