MAENDELEO BANK KUWAJENGEA NYUMBA WAMACHINGA DAR ES SALAAM,IKIWA NI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUINUA KIUCHUMI MAKUNDI MAALUMU
Katika kutambua jitihada zinazofanywa
na serikali za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa makundi maalumu wakiwermo
wamachinga Maendeleo Bank imezindua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa
Wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa Mei 7, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo Bank Dkt Ibrahim Mwangaraba wakati akizungumza na Waandishi wa habari,wakati wa utiaji saini kwa ajili ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo unaojulikana kama “Machinga Plot Finance’kwa ajili ya kuwakopesha viwanja vya makazi kwa bei nafuu.
"Ununuzi huu wa viwanja umeambatana na utiaji saini wa mkataba na makubaliano ya pamoja (Memorandum of Understanding) kati ya benki, Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) na mmiliki wa eneo husika," amesema Dkta Mwangalama kupitia taarifa yake kwa wanahabari
Aidha ameeleza kuwa hiyo ni dhamira ya Maendeleo Bank katika kukuza biashara kwa kuwekeza kwenye jamii hususan kwa makundi maalum wakiwemo wamachinga ili kuwainua kiuchumi.
"Leo tunashuhudia muendelezo wa huduma ya kipekee inayotolewa na Maendeleo Bank kwa Wamachinga, hakika tunajisikia fahari kuwa sehemu ya suluhisho la makazi kwa Wamachinga," ameongeza Mwangalaba.
Dkt.Mwangaraba amefafanua kuwa Septemba 2021, Benki ilianzisha bidhaa ya kuwawezesha wafanyabiashara ndogondogo waliopo Soko la Kariakoo na masoko mengine yaliyopo Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Chama chao kinachojulikana kama Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) chini ya bidhaa inayojulikana kama Wezesha Machinga.
Amesema kuwa walengwa wakuu ni wafanyabiashara wadogo ambao wametambuliwa na kuidhinishwa na Serikali kufanya biashara katika maeneo yaliyopangwa ndani ya masoko maarufu kwa jina la kizimba.
Amesema Madhumuni makubwa ya mkopo huo ni kuwawezesha wamachinga kupata mitaji kwa ajili ya kukuza biashara ambapo kupitia mkopo huo mmachinga ana uwezo wa kupata mkopo bila dhamana zaidi ya kizimba.
“Bank ilipokea maombi kutoka kwa KAWASSO ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa Wamachinga ambapo walikubaliana kuanza na ununuzi wa viwanja na hivyo kuwawezesha wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam kumiliki viwanja na hatimaye kupata makazi ya kuishi”.Amesema Dkt Mwangaraba
Aidha amesema kuwa umoja huo tayari umeshapata hekari 89 katika kijiji cha Magoza kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, na kwamba kupitia mpango huo Benki itatoa mikopo yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 500 kwa wamachinga karibu 500 kwa awamu ya kwanza ya mradi ili kuwawezesha kumiliki viwanja hivyo.
Dkt.Mwangaraba amesema ili kufanikisha lengo hilo, Benki kwa kushirikiana na KAWASSO, imeingia makubaliano ya pamoja na mmiliki wa eneo kwa upande mmoja na Benki, pia KAWASSO wameingia makubaliano na Kampuni ya urasimishaji ardhi inayojulikana kama Semsic Land Consultant Limited.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti KAWASO Namoto Yusuph Namoto ameishukuru Bank hiyo kwa kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuinua kundi la Wamachinga nakuahidi kushirikiana vyema katika kutekeleza mradi huo.
Namoto amesema kuwa mafanikio hayo yanatokana na uongozi mahili wa wamachinga uliopo kwa sasa ambao umehakikisha unawaratibu vizuri wamachinga kuwa na kanzi data ambayo inawafanya watambulike katika maeneo yao.
“Kariakoo tuna mitaa kumi na moja ya wamachinga,lakini pia tuna kanzi data ya kuwatambulisha wamachinga wote,pia tuna masoko kumi na saba katika halimashauri za wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es salaam,ndioa maana wenzetu Maendeleo Bank wanatupa mikopo kwasababu tunatambulika”amesema Namoto.




No comments
Post a Comment