JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZA OPARESHENI YA KUKAMATA MAGARI NA PIKIPIKI ZENYE VINGO"ORA KINYUME CHA SHERIA
Na Mussa Augustine
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini limesema litaanza Oparesheni kabambe ya kukamata Magari yote ambayo si ya dharula yliyofungwa vingora,Vimulimuli,Namba za Bandia,na taa za Kuongezwa kwenye vyombo hivyo vya moto bila kuzingatia utaratibu wa kisheria.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 23,2024 Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania DCP Ramadhani Nga’nzi Wakati akizungumza na waandishi wa habari nakusema kuwa Kuna baadhi ya watu wamejenga utamaduni wa kujihalalishia kuwa ni Sheria kuweka namba za bandia kwenye magari Yao.
Amewataka wamiliki na madereva wanaofunga vingora, vimulimuli namba za bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kama Kuna ulazima wa kufanya hivyo basi wanatakiwa kuomba na kupata ridhaa ya kufanya hivyo kutoka Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ndie mwenye dhamana ya kuidhinisha vibali hivyo.
“Wapo watu binafsi makampuni au taasisi zinafunga vingora katika magari yao na kubitumia bila kuzingatia utaratibu wa kisheria, Kwa kufanya hivyo wanaovunja sheria ya usalama barabarani na wanastahili adhabu ikiwemo ya kulipia faini ya tozo za makosa ya usalama Barabarani au kuweka mahabusu na kuandaliwa mashtaka na kupelekwa mahakamani au vyote Kwa pamoja” Amesema DCP Nga’nzi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni