Zinazobamba

DUKA LA VIATU AINA YA RELAXO LAFUNGULIWA DAR ES SALAAM ,MEYA KUMBILAMOTO AMPONGEZA MWEKEZAJI

 


Na Mussa Augustine.

Serikali imewahakikishia kuboresha zaidi mazingira ya usalama kwa Wawekezaji na kuendelea kuwapa ushirikiano ili kusaidia Serikali kutoa ajira za kudumu na za muda mfupi kwa wazawa .

 Akizungumza na Wanahabari leo Februari 20,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Duka la Viatu la Kampuni ya  Relaxo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam  Omary Kumbilamoto amesema Serikali peke yake haiwezi kutoa ajira kwa Vijana wote nchini.

 Kumbilamoto amesema panapotokea wawekezaji wengi inaleta faraja na mtazamo mzuri kuhakikisha Vijana wanaendelea kutafuta vipato vyao kupitia wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya Kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kuhakikisha zinapatikana fursa za ajira na viwanda vingi nchini.

Hata hivyo Meya huyo amesema kuendelea kuwepo kwa wawekezaji hao nchini ni ishara tosha kuwa usalama upo na umeimarishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam  SACAP Jumanne Murilo katika kuhakikisha anasimamia usalama  kwa Wawekezaji nchini

 Aidha Kumbilamoto ameipongeza Kampuni ya Relaxo kwa kupanga muda mzuri  wa kuuza bidhaa hizo hadi  muda wa usiku ili kuwapa nafasi watu wengi kufika katika maduka yao muda wowote  ili kupata huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya  Best brands Distributors ,Bw. Khalid Mohammed Salim amesema Kampuni yake imejipanga kuwafikia wateja wake kwa maeneo ya karibu na Jiji ambapo Tawi jipya la Relaxo lililopo mtaa wa Samora Posta Jijini Dar es salaam  litakwenda kuzalisha  ajira kwa vijana zaidi ya 50 kwa jiji la Dar es salaam ikiwa ni dhamira yao ya dhati ifikapo 2025 .

“Kipekee tumepata maombi mengi ukizingatia viatu vyetu tumelenga zaidi upande wa kimichezo hivyo wanamichezo wengi wanapenda kupata viatu vyenye ubora zaidi ndio maana tukawiwa kuendelea kufungua matawi katikati ya mji hili la leo tumezindua ni duka la tatu na tuna mpango wa kufungua  maduka 20 sanjari na ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa viatu hivyo ili kuwafikia wateja wetu kwa haraka kutokana na ubora wa viatu vyetu."amesema Salim

 Salim ameongeza kuwa viatu  vinayozalishwa vimesheheni viatu kwa rika zote na sehemu mbalimbali mahususi ikiwemo kwa matumizi ya mashuleni,hospitalini na sehemu zingine zenye matumizi ya viatu.

Pia amesema Kampuni hiyo imetoa ofa ya kuhakikisha watakaohitaji kuuza bidhaa hizo watagharamiwa fremu za biashara ili kuendelea kuzitangaza bidhaa hizo.

 

Hakuna maoni