Zinazobamba

TANESCO YAZINDUA PROGRAM YAKUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WAHANDISI


  Na Mussa Augustine

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka jitihada za kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake ili kuendana na sera ya serikali ya utekelezaji wa malengo ya kuongeza idadi ya wahandisi Wanawake ili kufikia dira ya Dunia ya asilimia hamsini kwa hamsini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gisima Nyamo_Hanga katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango maalum uwezeshaji unaolenga kuwajengea uwezo wahandisi wanawake, kuwaendeleza kiujuzi na kielimu, ili kukuza Maendeleo ya nchi.

Amesema, Mpango huo ni wa miaka minne na watashirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT),ambavyo watavitumia Vyuo hivyo kuwaendeleza kielimu wataalamu wakike washirika hilo, kusaidia kuwapata wanafunzi wanaohitimu fani ya uhandisi.

“Wahandisi wanawake katika sekta ya Umeme Ushiriki wao bado ni mdogo na sisi kama TANESCO tumeona ni muhimu kuja na mkakati maalum ambao utasaidia kuongeza wahandisi wengi wa kike ambao tutawaajiri na kufanya nao kazi kwani tunaamini mwanamke akipata elimu na akikabidhiwa na kupewa imani kufanya jambo lolote anafanya kwa uaminifu mkubwa na mafanikio makubwa mfano tunauona na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani” Amesema

Hata hivyo Mkurugenzi amebainisha kuwa Mradi huo unaratibiwa na Umoja wa Ulaya, lakini mpango wao wa mbele ni kuhakikisha kwamba unakua endelevu na hata baada ya huo mradi kuisha wao wenyewe wataendelea kuweka jitihada za kuendelea, lengo ni kuwapata wahandisi wengi wakike .

Ameongeza kwa kusema kuwa mradi huo umeanza na wanawake 40 ambao wanawezeshwa kielimu katika vyuo vikuu vya ndani na programu hiyo itakua ni ya miaka minne hivyo rai kwa wahandisi wakike kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika mpango huo.

“Mradi huo ni moja ya kichocheo cha kuwahamasisha watoto wakike kusoma fani ya uhandisi, mradi huu tumeanza na wanawake 40 lakini kila mwaka tutakua tunaongeza wengine,”amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk. Seif Shekalage, amesema hiyo programu iliyoanzishwa ni.jitihada ya kusaidia kuwapatia elimu.wanawake na kuwanufaisha kiuchumi wanawake ili nao waweze kuwa.katika nafasi nzuri serikalini
.

Sambamba na hayo amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maluum ipo tayari kushirikiana na TANESCO ili programu hiyo iwe mfano bora na wa kuigwa na taasisi na mashirika mengine nchini.

Nao wanufaika wa programu hiyo kutoka TANESCO, wameshukuru kupata fursa hiyo kupitia mradi huo kwani utawasaidia kuwaongezea ujuzi, ambao utawezesha kuongeza uzalishaji ndani ya shirika na kukuza Maendeleo ya Taifa.

Hakuna maoni