Na
Mussa Augustine.
Taasisi ya Watetezi wa Mama ambayo inajihusisha na Masuala ya
Kijamii,Siasa na Kiuchumi inatarajia kufanya shughuli mbalimbali za
kijamii katika kuelekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais Dkt Ras
Samia Suluhu Hassan itakayofanyika Januari 27 ,2024.
Hayo yamebainishwa Desemba 20,2023 na Msemaji wa Taasisi hiyo
Mkoa wa Dar es salaam Madebe Lidai wakati wa Mkutano na Waandishi wa
habari kuelezea namna Taasisi hiyo itakavyoshiriki ipasavyo katika
maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Dr. Samia Suluhu Hassan ambapo kauli mbiu
inasema " Mama ni Fahari sote tunajivunia".
"Januari 27 mwaka ujao ni siku ya kuzaliwa kwa Chifu
Hangaya( Rais Dr.Samia Suluhu) tunatarajia kufanya shughuli mbalimbali kuelekea
siku hii ikiwemo kutembelea vituo vya watoto yatima,vituo vya watu wenye
ulemavu,Wajawazito wasio na misaada hospitalini,pamoja na Wajane ili kuweza
kuyashika mkono makundu haya muhimu katika jamii" amesema Lidai ambaye ni
maarufu kwama Nabii Mswahili.
Sambamba na hilo Taasisi hiyo inatarajia kufanya ziara ya kutembelea
Miradi inayotekelezwa na serikali ya Dr Samia Suluhu Hassani kwenye halmashauri
za Manispaa zilizopo Mkoani Dar es salaam ili kuweza kuandaa Makala(
Documentary) itakayo onyeshwa siku ya kuzaliwa Dr.Samia Suluhu Hassan Januari
27 ,2024.
Awali Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mohamed Cassim Chande amesema
kwamba Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan amedumisha Amani na Mshikamano kwa
Watanzania hivyo Watanzania wanapaswa kumuunga Mkono katika jitihada zake za
kulinda tunu za Taifa.
"Sisi tuna deal( shughulika) na wale wanaobeza yale Mambo
Mazuri yanayofanywa na Rais Dkt Samia,hivyo napenda kutumia fursa hii kuwaomba
wale wote wanaofanya hivyo waache mara moja na 'Ukimvaa tutakuvaa kwa hoja'
amesema Chande kwa bashasha.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Watetezi wa
Mama William Frank Chitande amesema kwamba taasisi hiyo itaendelea kumuombea na
Kumsemea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya za
kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Hata hivyo afisa
Miradi wa Taasisi ya Watetezi wa Mama, Muhamad Sekamba amesema kwamba siku ya
kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kuzaliwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Michezo
mbalimbali itafanyika ikiwemo Jogging ,pamoja na bonanza la Mpira kati ya
Wasanii wa Bongo Movie na Waigizaji wa filamu ikiwa lengo ni kumuenzi Rais Dkt.
Samia kwa Mchango wake katika kukuza sekta ya Michezo nchini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni