Mkurugenzi wa MTWANGONET Fidea Ruanda
Na Mussa Augustine.
Imeelezwa kuwa moja ya
changamoto inazoikumba umoja wa Asasi za kiraia Mkoani Mtwara ( MTWANGONET) ni
ukosefu wa elimu ya uandaaji wa tariifa ya fedha za miradi zinazotolewa na
wafadhili hali inayopelekea kushindwa kuaminika kupewa tena fedha za miradi.
Kauli hiyo imetolewa tarehe
18,2023 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa MTWANGONET Fidea Ruanda, wakati
alipokua katika Semina ya kutoa tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Uraia Wetu
ambao unatekelezwa na wadau wa Asasi ya Foundation For Civil Society (FCS) chini ya
ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Fidea amesema kuwa,
lengo la mradi huo ni kuangalia mazingira wezeshi katika kutekeleza majukumu
yake na kushirikiana na Serikali ambapo wanatekeleza mradi huo katika mikoa
saba ikiwemo Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Mtwara, Rukwa, ambapo
wanasimamia Kanda ya kusini katika mradi huo huku ukilenga kwa vijana,
wanawake, na walemavu ambapo unatekelzwa kwa miaka 3 kuanzia 2023 hadi 2025.
"Uwelewa mdogo
kuhusu sera, sheria na miongozo mbalimbali ikiwemo kulipa asa kwa mashirika
machanga bado ni changamoto licha ya kuwa malipo ni shill 50,000 kwa mwaka
kwani usipolipa hadi kufikia mwezi wa April mwaka unaofuata unapigwa faini
asilimia 100 ambapo ni sawa na shill laki 100,000" amesema Fidea.
"Tunatakiwa tuwe
na umoja wetu tuongee kauli moja ,tuwe na agenda moja ya mradi wetu ili
kuangalia namna ya kuuendesha mradi kwani lengo ni kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuboresha maisha ya wananchi" amesema Fidea
Mratibu wa Miradi kutoka FCS Nicholas Lekule
Kwa upande wake,
Mratibu wa Miradi kutoka FCS Nicholas Lekule amesema kuwa, FCS imetoa ruzuku
kwa wadau kumi na tano ambao wanafanya kazi katika maeneo tofauti tofauti
ikiwemo kwenye kanda, kitaifa na zile asasi zinazofanya kazi na wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu, huku wadau 12 wakipokea shill mill 110, na wadau
3 wa kitaifa wakipokea shill mill 145.
Aidha, amesema kuwa
tathmini ya mradi wa Uraia Wetu iliyofanyika leo nikutaka kuangalia lengo
lake ikiwa ni kuwajengea uwezo katika asasi za kiraia ziweze kufanya shughuli
ambazo zitasaidia kuleta mabadiliko ya kisera.
"Moja ya kazi tunazofanya nikuziboresha
asasi za kiraia ili ziweze kufanya kazi zenyewe ili kukabiliana na changamoto
zinazojitokeza,leo watatuonyesha wao ni akina nani wamekutana na akina nani
katika kutekeleza mradi huo,nichangamoto zipi na nikwanamna gani wanashirikiana
na serikali na watunga sera katika kufanya kazi" amesema Nicholas
Hakuna maoni
Chapisha Maoni