Zinazobamba

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi  Paul Makonda amesema kwamba Maoni ya Wananchi  juu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa kwa Miaka thelathini ni muhimu hivyo amewaomba  wananchi  kujitokeza kwa wingi katika utoaji wa maoni kwa tume maalumu iliyoundwa kukusanya maoni hayo.

Hayo ameyasema Desemba 21,2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kutoa tathmini ya robo Mwaka ya CCM ambapo  amesisitiza  kuwa tayari sheria imeshapitishwa na  bunge hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kutoa maoni ya nini anataka kiwekwe katika dira hiyo 

"Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika suala zima la utoaji wa maoni ya nini wanachotaka kiwekwe kwenye dira ya Maendeleo ya Taifa , na Mpango huu utawafikia wananchi wote kwa sababu tayari tume maalum imewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni hayo',amesema .

 

Sambamba na hayo  katibu huyo Mwenezi wa CCM ameonyeshwa kukerwa na  na kitendo cha ukatikaji wa umeme mara kwa mara na kuwataka viongozi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO)kujitathimini bila kusubiri kuchukuliwa hatua.

 

 Amesema hivi karibuni Tanesco wamemuahidi Rais Samia ya kwamba ifikapi Januari kuwa kinu cha umeme kitawashwa hivyo ni vyema ahadi hii ikatekelezwa kwa vitendo.

 

Aidha amewataka watendaji wote kuanzia ngazi shina hadi mkoa kusikiliza kero za wananchi Ila kutatua changamoto zinazowakabili.

 

" Nataka niwakumbushe ndugu viongozi tuliopewa dhamana Na Rais Samia ya kuwatumikia wananchi ni vyema tukatekeleze wajibu wetu tusisubiri mpaka Rais Samia anzishe ziara aanze kasimamishwa njiani na wananchi ili watoe malalamiko yao,"amesema Makonda.

 

Akizungumzia suala la kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa Makonda amesema ni vyema wanachama wenye nia ya kugombea uongozi kuacha viongozi waliopo madarakani waendelee kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao bado ni viongozi Halali wanaotambulika kisheria.

 

"Najua wapo watu ambao wameanza kampeni za hapa Na pale Mimi niwambie tu ndugu zangu waacheni viongozi wafanye kazi kwa sababu muda wao haujaisha Na wao bado ni viongozi wanaotambulika na bado wanahaki ya kuwatumikia wananchi", amesema Makonda.

 

Hata hivyo Pauli Makonda  amebainisha kuwa kuanzia Januari 13 /2024 ataanza ziara ya kikazi katika mikoa 10 ikiwemo  Tanga,Pwani,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Singinda,Tabora,Shinyanga  na Simiu.

 

Ambapo amewataka watendaji wa halmashauri zote watakaopitiwa na ziara hiyo waanze kujitathmini kabla ya kiongozi huyo kupita maeneo hayo.

 

 

 

Hakuna maoni