Zinazobamba

DCEA YATOA ONYO KALI KWA WANAOFANYA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.

     Kamishna Jeneral wa DCEA Aretas Lyimo 

Na Mussa Augustine.

 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya  DCEA imetoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya Dawa za kulevya nchini Tanzania badala yake wajikite kwenye biashara nyingine halali kwani Mamlaka hiyo imejidhatiti kukomesha biashara hiyo kwa kufanya oparesheni katika maeneo mbalimbali nchini. 

Onyo hilo limetolewa Desemba 27,2023 Jijini Dar es salaam na Kamishna Jeneral wa DCEA Aretas Lyimo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa habari kuelezea Mafanikio ya oparesheni maalumu inayofanywa na Mamlaka hiyo katika kudhibiti biashara ya Dawa za Kulevya Nchini.

 Kamishna Lyimo amesema kwamba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania DCEA imekamata jumla ya kilogram 3182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya tarehe 5 hafi 23 mwezi Dicemba mwaka 2023.

Aidha ameendlea kusema kuwa kuwa katika oparesheni hiyo jumala ya watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia.

 Amesema kuwa,kiasi hiko cha dawa za kulevya ambacho hakijawai kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.

Aidha amesema kwamba Kiasi hicho cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180,29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika wilaya za kigamboni, ubungo na kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa Mkoani Inringa.

 Aidha, dawa hizo zilizokamatwa zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio zenye chapa mbalimbali za kahawa na majaninya chai ambapo mbinu hiyo inatumika kwa lengo labusafirishaji wake na kukwepa kubainika.

 Hata hivyo, amesema kuwa dawa aina ya methamphetamine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa cocaine ambapo dawa hiyo huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembembe mithili ya chunvi ang'avu yenye rangi mbalimbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubukwa kuchanganya aina mbalimbali za kemikali bashirifu.

 "Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji madhara yake ni makubwa na hayatibiki kirahisi kwani mtumiaji hupata madhara ya kudumu kwenye ubongo na hivyo hupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu kusababisha uraibu na kuathiri mfumo mzima wa faham;.Amesema Kamishna Lyimo

 Kamishna huyo ameongeza kuwa, kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa zingefanikiwa kuingia Mtaani zingeweza kuathiri zaid ya watu 76, 368,000 kwa siku hivyo, ukamataji huo umeokoa nguvu kazi ambayo ingeangamia kutokana na madhara yatokanayo na madawa ya kulevya ndani na nje ya nchi.

 Katika hatua nyingine Kamishna Lyimo  ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka hiyo katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi mkubwa.

Hakuna maoni