Zinazobamba

RAIS DKT SAMIA KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA KWANZA WA KITAIFA WA DIRA YA MAENDELEO.


Na Mussa Augustine.

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ambao utafanyika Disemba 9, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa ( JNICC ) jijini Dar es Salaam. 

 Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ,ambapo amebainisha kuwa lengo la Mkutano huo ni kuzindua, kupokea na kujadili taarifa ya kitafiti ya Tathmini ya utekelezaji wa Dira ya taifa ya maendeleo 2025.

 Profesa huyo amesema kuwa, taarifa ya kitafiti ya tathimini ya utekelezaji wa Dira ya taifa ya maendeleo 2025, pamoja na mambo mengine imeanisha mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa dira ya kwanza ya taifa ya maendeleo.

 "Dira hii ilianza kutekelezwa mwaka 2000 na itafikia mwisho wake mwaka 2025, pamoja na mafanikio mengine, taarifa ya tathmini inaonesha kuwa pato la Mtanzania limeongezeka kutoka dola za kimarekani 399.5 sawa na shill 322,597 kwa mwaka 2000 hadi kufikia dola za kimarekani 1,200 sawa na shill 2,880,000 kwa mwaka 2022 "amesema Waziri Kitila.

 Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imefikia asilimia 124 ya kujitosheleza kwa chakula ikilinganishwa na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo mwaka 2025, ambapo hatua hiyo imewezesha Tanzania kukabiliana na njaa kwa mikoa na wilaya zote nchini. 

 Amesema kwamba mtandao wa barabara za lami na zege katika mikoa umongezeka kutoka kilometa 4,179 mwaka 2000 hadi kufikia kilometa 11,966,38 mwaka 2023, ambapo mafanikio mengine ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 760 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2000 hadi kufikia vifo 140 mwaka 2022. 
 Hata hivyo, amesema mkutano huo pia Rais Samia atazindua rasmi timu kuu ya kitaalam ya dira na kamati ya usimamizi wa dira pamoja na nyezo za kidigital zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wadau.

 "Kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia zoezi la kuandaa dira mpya ya maendeleo liwe jumuishi na shirikishi, mkutano huu utahudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka pambe za nchi yetu, wadau hawa ni pamoja na viongozi wakuu wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, 
Mawaziri,viongozi wa dini,watu wenye ulemavu, wazee pamoja na kilimo"amesema Waziri Mkumbo. 

Sanjari na hayo siku hiyo Rais Samia anatarajiwa kutumia siku hiyo kutoa ujumbe maalum katika kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Hakuna maoni