WANANCHI KATA YA TABATA WAILALAMIKIA KAMPUNI MPYA YA UZOAJI TAKA.
Taka ambazo zimelundikwa kwenye chumba maalumu kutokana na kushindwa kuzolewa kwa wakati katika Mtaa wa Tenge Kata ya Tabata.
Na Mussa Augustine.
Wananchi
wa Kata ya Tabata Manispaa ya Ilala Mkoani Dar es salaam wameilalamikia Kampuni
ya PB URASA LOGISTICS ambayo imepewa zabuni ya kuzoa taka kwa kushindwa kuzoa taka kwenye mitaa yao
tangu Kampuni hiyo ipewe kazi hiyo Novemba Mosi ,2023.
Malalamiko
hayo wameyatoA Novemba 15,2023 kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na
waandishi wa habari waliotembelea katani humo kujionea adha wanayoipata
Wananchi hao ikiwemo harufu mbaya itokanayo na taka hizo hali ambayo pia
inahatarisha afya zao kutokana na mripuko wa magonjwa ya kipindupindu.
“Tangu
mwezi huu wa kumi na moja uanze sijawahi kuona gari la taka linapita kuzoa
taka,nalipa hela ya taka kama kawaida lakini sipati huduma ,angalieni humu
ndani taka zimejaa hadi funza wanatoka
hii ni hatari sana kwa afya yetu “amesema Bibi Lulu ambaye ni Mkazi wa
Mtaa wa Tenge uliyopo katika kata ya Tabata.
Nae
Linah Shayo mkazi wa Tabata Bima Mtaa wa Mengwe amebainisha kuwa hana taarifa
kama kuna Mkandarasi mpya ambaye amepewa Zabuni hiyo nakwamba wananchi wanapaswa kushirikishwa kutoa maoni yao pindi
Mkandarasi mpya anapotafutwa ,lakini kwa Mkandarasi Mpya PB URASA LOGISTICS
aliyepo kwa sasa Wananchi wanadai hawajashirikishwa na uongozi wa kata hiyo.
“Sisi
tunatoa pesa zetu bila shida lakini Mkandarasi aliyeletwa kwa sasa hatoi taka
kwa wakati,pia anabagua wenye pesa nyingi(matajiri) wanapata huduma kwa wakati
lakini sisi Maskini ambao tunatoa pesa kidogo hatupewi huduma “amezungumza kwa
uchungu Linah mbele ya Waandishi wa habari.
Nakuongeza
“gari likipita taka zetu zinakua nje lakini zinaachwa hivyo inatubidi tena
kuzirudisha ndani,hatuelewi ana maana gani huyu Mkandarasi mpya (PB URASA
LOGISTICS) au anataka tutupe hizi taka barabarani ,tupeni ruhusa tutupe
tumechoka”amesema Linah
Stanley
Harold Mkazi wa Mtaa wa Umoja Road Mkandarasi aliyesitishiwa Mkataba wake (BUSAE
COMPANY LTD )hakua na tatizo lolote katika utoaji huduma kwa Wananchi kwani alikua
akifika kwa wakati kutoa taka hizo tofauti na aliyepo kwa sasa ambaye amesema
inawezeka hana vitendea kazi vya kutosha.
“Inawezekana
ni hila tu wamemfanyia mkandarasi wa zamani,lakini Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni Mkandarasi wa Zamani(BUSAE
COMPANY LTD )alikua na Vitendea kazi vya kutosha na alikua anatimiza wajibu
wake ipasavyo,inawezekana kuna tofauti zao na viongozi wa kata yetu ,ndiyo
maana wamemtoa lakini sisi wananchi tunaomba waondoe tofauti hizo wamrudishe
mkandarasi wa zamani”amesema Stanley
Hata
hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Tabata aliyefahamika kwa jina moja la Mapesa
hakua tayari kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo kwa madai kuwa mwenye
mamlaka ya kuzungumzia sakata hilo ni Mkurugenzi wa Jiji la Dares salaam.
aka ambazo zimelundikwa kwenye chumba maalumu kutokana na kushindwa kuzolewa kwa wakati katika Mtaa wa Tenge Kata ya Tabata.
Kwa
upande wake Meneja wa Kampuni ya Zamani iliyositishiwa Mkataba Oktoba 31,2023 ya
BUSAE COMPANY LTD Faraja Adamu amebainisha kuwa walipata barua kutoka ofisi ya
Mtendaji wa Kata hiyo ikiwataka kusitisha huduma ya kuzoa taka katani humo bila
kuelezwa sababu zilizopelekea kufikiwa kwa maamuzi hayo.
“Hatujui
sababu ni nini mpaka tunasitishiwa mkataba ,kama kulikwa na dosari tungeelezwa
lakini tumeshangaa analetwa mkandarasi mpya ambaye tangu tarehe 1,mwezi huu wa
11 hajazoa taka na hali ni mbaya mtaani,Wananchi wanatupigia simu sisi kwani bado
wanajua kuwa tunatoa huduma”amesema
Fraja.
Nakuongeza
kuwa mwezi wa kumi tumeingiza magari mengi barabarani kuzoa taka,na kila mtaa
ambao tumepita wenyeviti wa mtaa walikuawa wakisaini dispachi
yetu,tumesitishiwa mkataba tukiwa tumeshazoa taka zote na mwezi huu wa kumi na
moja tunaendelea na ukusanyaji wa madeni ya fedha za taka kutoka kwa wanachi ambazo niza huduma ya mwezi wa kumi.
Aidha
Faraja ameongeza kuwa wamepewa siku kumi
na tisa pekee za kukusanya fedha hizo huku akidai kuwa kwa utaratibu wanapaswa kupewa siku thelathini za kukusanya
fedha hizo yaani kuanzia Novema 1 hadi Novemba thelathini mwaka huu,hivyo
wameiomba ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaa kuingilia kati sakata
hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni