Zinazobamba

CHIFU SANGALALI AWAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA MATEMBEZI YA AMANI YA JMAT.

Na Mussa Augustine.

Mwenyekiti wa Machifu Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Nchini humo( JMAT) Chifu Antonia Sangalali amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika Matembezi ya Amani yatakayofanyika Desema 2 ,203 jijini Dar es salaam.

Rai hiyo ameitoa Novemba 21,2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi  habari ikiwa ni mwendelezo wa kutoa taarifa ya maandalizi ya Matembezi hayo yenye lengo la kuiunga Mkono Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hasssan katika kudumisha Amani Nchini.

“Mimi ni chifu wa kabila la Wasukuma Mkoani Simiyu lakini pia ni Mwenyekiti wa Machifu Tanzania,pia ni Mjumbe wa JMAT ,hivyo katika matembezi hayo kutakuwepo na tisheti maalumu ambazo tutazivaa kwa yeyote anayehitaji zinapatika hapa ofisi za JMAT na utaratibu wa kuzipata utatangazwa na uongozi  “amesema Chifu Antonia.

Nakuongeza kuwa”naomba wanachi wajitokeze kwa wingi katika matembezi hayo ili tumuunge mkono Rais Wetu Mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhimiza kwa vitendo kudumisha amani katika Taifa letu,kwani amani inatokana na sisi wenyewe.

 

Hakuna maoni