UONGOZI MPYA TCCIA UMEAHIDI MAGEUZI MAKUBWA YA MAENDELEO SEKTA BINAFSI
Na Mussa Augustine
Rais Mpya
wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA) Vicent Bruno Minja amesema
kuwa uongozi wake unatarajia kufanya mambo makubwa ndani ya siku miamoja ikiemo
kuimarisha Ushirikiano wa dhati kati ya Wanachama ,Wafanyabiashara na Wadau
wote ili kuhakikisha sauti za wanachama zinasikika na kuzingatiwa katika kila
hatua inayochukuliwa.
Hayo
ameyasema Novemba 10,2023 Jijini Dar es salaam wakati akizungmza na waandishi wa habari kwa
lengo la kutangaza rasmi bodi mpya ya TCCIA iliyochaguliwa hivi karibuni kupitia Mkutano
Mkuu Maalumu uliyofanyika Novemba 7 ,2023 jijini humo.
Aidha Rais Minja amesema kuwa Mwelekeo na Mpango Mkakati wa uongozi huo ni pamoja na Kukuza
Maendeleo ya Sekta za Biashara,Viwanda na Kilimo kwa kushirikiana na Serikali
na Wadau wengine kwa kuweka mikakati imara ya kuvutia uwekezaji,kutoa mafunzo
na kusaidia miradi inayochangia ukuaji wa sekta hizo muhimu.
Rais huyo wa
TCCIA amendelea kutaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na Kuendeleza Ubunifu na
teknolojia katika utoaji wa Vyeti Vya uasili,Kukuza Umoja na Mshikamano ndani
ya Chemba ,Kuimarisha ushirikiano na Serikali ,Taasisi ,Balozi na Wadau wa
Maendeleo ,Kusimamia Mabaraza ya Biashara na Kuendelea kuhudumia Sekta Bianafsi
Nchini.
''Tutatumia
uzoefu wetu wa miaka 35 katika huduma na uongozi wa sekta Binafsi nchini
kusimamia Mabaraza ya Biashara na kuendelea kutoa huduma bora kwa sekta
binafsi'',amesisitiza Rais Minja.
Kwa Upande
wake Makamu mpya wa rais Sekta ya Kilimo Swallah Swallah amesema kuwa Sekta ya
Kilimo ni Muhimili Muhimu wa TCCIA,nakwamba asilimia karibia kubwa ya Wananchi
wapo katka sekta ya kilimo hivyo Chemba hiyo itashirikiana na serikali
kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za kilimo kwa wakati lakini pia kupata masoko ya uhakika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni