DKT ALHAD MUSSA AWASIHI WANANDOA KUISHI KWA UAMINIFU
Hayo yamesemwa
Oktoba 31,2023 na Sheikh Dkt.Alhad Mussa alipozungumza na Waandishi wa habari ofisini kwakwe Jijini Dar es salaam,kufuatia kuwepo kwa tatizo kubwa la wanandoa kwenda katika vituo vya afya
kupima DNA za watoto kwakile kinachoitwa kukosekana kwa uaminifu baina ya
wanandoa.
“Kwanza
watanzania hawanabudi kutambua kwamba ninayoyasema ni kwa niaba ya JMAT na si
vinginevyo wakati uliopita nilikuwa nina kofia mbili hii ya JMAT na ya Sheikh
Mkoa wa Dar es Salaam, lakini sasa nazungumza kwa niaba ya Taasisi kubwa,tatizo
lipo, kikubwa nikuwa na hofu ya Mungu,tukiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu tutakuwa
salama pasipo hivyo kuiona pepo itakuwa aghalabu” amesema Sheikh Dkt .Alhad Mussa
Amesema
dhambi ifanywayo na binadamu wa karne hii ni kufulu zaidi ya ile ya Sodoma
na gomora, kwakuwa imefikia mahala sasa wanaume kwa wanaume wanahitaji kufunga
ndoa kwa kile wanachokiita haki za binadamu ni upuuzi na ujinga kwa binadamu
waliostaarabika ,sodoma walifanya kwa siri sasa ni bayana jambo ambalo halikubaliki
mbele za Mungu.
Aidha
Sheikh Dkt Mussa amesema ili kuepuka dhambi itokanayo na zinaa,wanandoa wote
wawili wa kiume na kike hawanabudi kuachana na tabia mbaya ya kutoka nje ya
ndoa,kwani dhambi hiyo ni kubwa kuliko wanandoa wanavyofikiria kwao ni dogo,
lakini wanayemkosea halioni dogo na adhabu yake siku ya kiama ni kubwa.
Vilevile
amesema yapo makosa yanayofanywa na wanaume kwa hoja ambazo hazina mashiko hata
kidogo, kumbagugua au kumkataa mtoto kwa kigezo cha rangi na maumbile, hadi
kufikia kupima DNA bahati nzuri awe wake asipo kuwa wake atakuwa ameathirika
kisaikolojia kwa kiasi kikubwa.
Sheikh
Dkt Mussa ameongeza kuwa kadhia kubwa katika wimbi hili kubwa la watu kupima
DNA ni kutoaminiana baina ya wanadamu huku akiwaomba watanzania kuzingatia
tamaduni za nje na kitanzania ambazo ni nzuri.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni