Zinazobamba

WAZIRI SLAA ATOA SIKU SABA KUTATUA KERO ZA URASMISHAJI WA ARDHI DAR ES SALAAM

 

Na Mussa Augustine.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kushughukia kero ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa huo.

Waziri Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mkoani Dar s salaam  ametoa maagizo hayo Oktoba 4,2023  jijini Dar es salaam wakati alipokutana na Wataalamu wa Ardhi,Viongozi wa chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Dar es salaam,Madiwani,Wabunge na Wakuu wa Wilaya  pamoja na Wataalamu wa Ardhi kutoka halamshauri za Mkoa huo,

kwa  lengo la kujadiliana namna ya kutatua tatizo la urasmishaji wa ardhi linalofanywa na baadhi ya Makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha kutoka kwa wananchi huku yakishindwa kutekeleza kazi hiyo kwa wakati.

Aidha Waziri huyo wa Ardhi  ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua kero hiyo nakwamba baada ya hapo wawasilishe taarifa kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam.

"Tatizo la Urasmishaji ni kubwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako  tukitoka hapa kwenye kikao Mkaanze kushughulikia tatizo hili ndani ya siku saba ,halafu mlete taarifa kwa viongozi wa chama,pia kama kuna tatizo la fedha mniambie ili tuone tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii" amesema Waziri Slaa

Waziri Slaa amesisitiza kwamba hataki kuskia kero za urasmishaji wa ardhi  zinaendelea kujitokeza katika uongozi wake nakwamba makampuni yanayojihusisha na urasmishaji huo yanapaswa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria nakwamba yale yatakayoenda kinyume yachukuliwa hatua za kisheria .

"Serikali imepanga kupima na kutoa hati za ardhi milioni mbili na laki tano(2.5 milioni) kufikia 2025,hivyo lengo la serikali ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kwasasa mikoa yote ishirini na sita(mikoa 26) nchini kuna makamishna wa ardhi wanaotoa hati ,hatua hii inasaidia wananchi kupata hati zao bila usumbufu" amesema 

Nakuongeza kwamba "Urasmishaji umekua tatizo kubwa katika simu kumi ninazopigiwa na wananchi simu saba hadi nane zinahusu malalamiko ya urasmishaji wa ardhi,sasa hapa nimekuja na timu yangu inayohusika na mambo ya ardhi napenda kuagiza kuhakikisha kero hizi zinashughulikiwa haraka sana".

Awali akizungumza  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu amesema kwamba Mkoa wa Dar es salaam umekua na tatizo la urasmishaji kutokana na kazi hizo kupewa makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha za wananchi nakutokomea nazo bila kufanya kazi hiyo kwa wakati.

“Kutokana na tatizo hili kuwa kubwa tumeona tukuite mheshimiwa Waziri najua hata wewe kwenye jimbo lako la Ukonga tatizo hili nikubwa,nakuomba utupe maelekezo yako ili kuondoa tatizo hili " amesema Mtemvu kwenye mkutano huo.


Hakuna maoni