S3 EDUCATION YATOA FURSA KWA WANAFUNZI WA KITANZANIA KUTAFUTA VYUO VIKUU NJE YA NCHI.
Na Mussa Augustine.
Katika
kuunga Mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukuza
sekta ya Elimu, taasisi inayojihusisha na Masuala ya Maonyesho ya Elimu ya Vyuo vikuu S3 Education imefanya maonesho hayo kwa kukutanisha vyuo vikuu mbalimbali kutoka nje ya Nchi.
Akizungumza Oktoba 10 ,2023 Katika Maonesho hayo yaliyofanyika
katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam,Meneja wa Taasisi hiyo, Fatema
Salemwalla, amesema kuwa Maonesho hayo yatawasadia wanafunzi kupata uelewa
mpana wa kozi ambazo wanahitaji kwenda kuzisoma nje ya nchi kwa kukutanisha
moja kwa moja na wahusika wa vyuo hivyo.
Aidha Fatema
amesema kuwa Kwenye Maonesho hayo zaidi
ya wanafunzi 500 kutoka shule mbalimbali wametembelea katika mabanda ya vyuo hivo nakuweza kujionea
fursa mbalimbali za kielimu kutoka katika vyuo vikuu vya Nje ya Nchi ya Tanzania
ikiwemo Vyuo Vikuu vya nchini
Mauritius,UK,Canada,USA,pamoja Ujerumani.
"Maonesho
haya huwa tunayafanya mara mbili kwa mwaka,lengo ni kutoa fursa kwa vyuo hivi
vikuu nje ya nchi kutangaza kozi zao,tunawaalika wanafunzi kupitia shule zao
kuja kutembelea maonesho haya,na sasa hivi teknolojia imekuwa kubwa,wanafunzi
wanafanya utafiti mapema wa kujua kozi ambazo wanahitaji kusoma kabla hata
hawajafika kwenye vyuo husika"amesema Fatema na kuongeza kuwa,
"Tupo hapa
na idadi ya vyuo vikuu 12 kutoka nje ya nchi ambavyo vimeshiriki Katika
maonesho haya na tunahitaji tuendelee kutafuta vyuo vingine zaidi ili kutoa
fursa kubwa zaidi kwa wanafunzi wa Kitanzania kutimiza ndoto zao za kielimu
kwenda kusoma nje ya nchi"
"Leo
tumepata fursa kubwa ya kutambua vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi ambavyo vina
kozi tunazozipenda na wazazi wetu wanao uwezo wa kuvilipia ambavyo vitatupa
elimu ambayo itatupa mwanga wa kuja kuwekeza hapa nchini Tanzania"amesema
Maryam
Hakuna maoni
Chapisha Maoni