Zinazobamba

SHEIKH DKT. ALHAD MUSSA AHIMIZA KUDUMISHA AMANI TANZANIA

                    Sheikh Dkt Alhad Mussa Salum

 Na Mussa Augustine.

Mwekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania(JMAT) Sheikh. Dkt Alhad Mussa Salum ameiomba Serikali na  Watanzania kwa ujumla kuendelea  kudumisha Amani ili kuepukana na hatari ya kuingia katika Machafuko yanayoweza kusababisha vita.

Sheikh Dkt Alhad Mussa ametoa Wito huo  Oktoba 12 Jiji Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kufuatia ziara yake nchini Korea Kusini,Kenya na Iran, ambapo ziara hiyo ilikua ni kuhudhuria mkutano wa Amani wa Kimataifa ambao uliwahusisha viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa Amani kutoka ulimwenguni kote,na umefanyika jijini Seoul Nchini Korea kusini.

 Aidha amesema kwamba kufuatia Mkutano huo amejifunza Mambo Mengi ikiwemo Umuhimu wa kulinda Amani kwani Mataifa ya Korea Kusini na Iran hayataki kusikia  uvunjifu wa amani na Vita  kwasababu yamepata athari  kubwa kutokana na Vita,hivyo ameiomba jamii iendelee kushirikiana kudumisha Amani.

 "Korea Kusini na Iran hawataki kusikia kabisa uvunjifu wa Amani na Vita ,wanajua vita ni kitu kibaya sana ,sisi hapa Tanzania Wakristo na Waislam tunavumiliana tuendelee kudumisha amani ya Taifa letu" amesisitiza Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum ambaye kwenye ziara hiyo aliambatana na  Mratibu wa JMAT Taifa Bi. Fatma  Kikkides pamoja na Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Mipango,Fedha,Uchumi na utekelezaji Joseph Sanga.

 Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa JMAT amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Falsafa kutoka chuo kikuu kilichopo nchini India kufuatia ziara ya Kitaifa  aliyoifanya hivi karibuni nchini India.

 "Watanzania tumuunge Mkono Rais wetu Dkt.Samia Saluhu Hassan ,tumtie moyo afanye kazi zake kwa heshima na utulivu katika kutuletea maendeleo " amesema Sheikh Dkt Alhad Mussa kwanye Mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

           Katibu Mkuu wa JMAT Askofu Dkt Isrel Ole-Gabreil Maasa

Awali akisoma taarifa ya Ziara ya Mwenyekiti wa JMAT Taifa Nchini Korea Kusini,Kenya na Iran Katibu Mkuu wa JMAT Askofu Dkt Isrel Ole-Gabreil Maasa amesema kwamba Mkutano huo Umeleta faida kubwa kwa baraza hilo kwani wameweza kujenga mahusiano ya kimataifa na shirika la  kimataifa linalojihusisha na Masuala ya Amani Duniani ( HWPL) kwa kusaini Mkataba wa Mashirikiano juu ya masuala ya Amani Duniani.

 "Mkutano huu ulifanyika jijini Seoul Korea kusini kuanzia tarehe 17 hadi Agost 19,2023 ,Mkutano uliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Amani lijulikanalo kama Heavenly Culture World Peace Restoration of Light ( HWPL) hivyo JMAT ilishiriki kikamilifu,nakuweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo Mratibu wetu wa Taifa Bi.Fatma Fredrick Kikkides kupewa Ubalozi wa Amani Duniani kupitia Shirika tanzu la HWPL linaloshughulikia Amani kwa wanawake liitwalo International Women Peace Group( IWPG)" amesema Askof  Dkt. Maasa 

 Nakuongeza kuwa Mwenyekiti wa JMAT Taifa pia alifanya ziara ya Kikazi Nchini Kenya mnamo tarehe 26 ,09 , 2023 baada ya kupatiwa mwaliko wa kuwa mgeni rasmi jijini Mombasa katika shughuli ya kumtawaza Mufti Mpya wa Kenya Sheikh Mshali Khamis Mshali Ashiraazy kupitia taasisi ya Kemnack Nchini Kenya.

 "Jambo hili limeiletea heshima kubwa JMAT na heshima kwa Mwenyekiti wetu pia,ambapo katika Safari hii Mweyekiti Dkt. Alhad Mussa Salum aliambatana na Maofisa kadhaa kutoka Makao Makuu JMAT Dar es salaam.

 Hali kadhalika Askof Dkt. Maasa amebainisha kuwa Mnamo Septemba 30 ,2023 Mwenyekiti wa JMAT Taifa alipata mwaliko wa kuhudhulia mkutano wa Umoja wa Umma wa kiislam na Mahusiano ya Dini mbalimbali jijini Tehran Nchini Iran, Mkutano uliofunguliwa na Rais wa Iran Mheshimiwa Ayatollah Sayyid Ibrahim JMAT.

 "Kwenye Mkutano huo Mwenyekiti wa JMAT Taifa alipata nafasi ya kutoa Hotuba juu ya masuala ya Umoja wa Kiislamu na Mahusiano ya Dini mbalimbali pia aliongea na vyombo vya habari Nchini humo ,pamoja na JMAT kuongeza  marafiki wengi wa kimataifa ambao tunaweza kushirikiana nao juu ya Masuala mbalimbali yanayohusu Amani Duniani" Amesema Askofu Dkt Israel.

 Kwa upande wake Mratibu wa JMAT Taifa Fatma Kikkides ambaye pia ni balozi wa Amani ,amesema amejifunza mengi Nchini Korea kusini na hivi sasa anaendelea na mafunzo maalumu juu ya amani baada ya mafunzo hayo atajikita zaidi katika kutoa mafunzo ya kulinda amani kwa wanawake na jamii kwa ujumla.

"Nimejifunza Mambo Mengi Sana, Wanawake na Watoto ndio wanaoathirika sana inapotokea vita,nina mambo mengi yakuelimisha jamii ,mikakati yangu mafunzo yakikamilika nitaendelea kutoa elimu kwa jamii kudumisha Amani ya Taifa" amesema Bi.Fatma kwa bashasha kubwa.

 Nae Mkurugenzi wa Dini JMAT Askof George Paul Fupe amesema kwamba JMAT imekua yakimataifa  kutokana na kusaini mkataba wa ushirikiano na Korea kusini,hivyo ameihimiza jamii kulinda Amani ya Taifa kwani amani ni tunu adimu.

 


Hakuna maoni