Zinazobamba

JESHI LA POLISI LAIMARISHA MIFUMO YA USALAMA KUELEKEA MECHI YA SIMBA & AL ALHY.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani).

Na Mussa Augustine.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani,nakwamba atakayefanya  hivo  kisheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jummane Muliro amesema kuwa Jeshi  hilo linatambua kuwa Ijumaa, Oktoba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam kutakuwa na uzinduzi Mashindano ya“African football league”

 ambapo pia kutakuwa na mchezo wa soka hatua ya robo fainali ya mashindano hayo baina ya klabu ya Simba ya Tanzania na Al Ahly ya nchini Misri utakaochezwa kuanzia majira ya saa 12:00 jioni,ambapo mifumo ya Usalama imeimarishwa.

 SACP Muliro amesema kuwa, jeshi la Polisi linatambua mchezo huo utahusisha wageni kutoka nje ya nchi na kuwa na mkusanyiko mkubwa katika kiwanja hicho, kutokana na hali hiyo  baadhi ya barabara zitafungwa ili kupunguza msongamano wa kuelekea uwanjani hapo, hivyo mashabiki wa soka wafike mapema ili kuepusba usumbufu unaoweza kuepukika.

 "Jeshi la Polisi limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo, ukaguzi wa hali ya juu katika mageti ya kuingia na hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo"amesema  

 Ameongeza kuwa,mtu yoyote asiyekuwa na tiketi hataruhusiwa kusogelea uwanja huo au maeneo ya milango ya kuingia ili usalama uimarishwe zaidi kutokana  na uhalisia wa kuwepo kwa watu wengi uwanjani hapo.

 SACP Muliro ameongeza kuwa jeshi la polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFFtabia ambazo zinaweza kupelekea Tanzania kukosa sifa yakuandaa mashindano kama haya wakati mwingine.

 "Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka kushangilia kistaarabu nakuacha alama nzuri ya kiusalama Katika Taifa la Tanzania" amesisitiza kwenye Mkutano huo na Waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam SACP Muliro amewataka Mashabiki wanaoingia na watoto Uwanjani kuacha kuingia na watoto ambao hawana tiketi kwana wanakua hawana sehemu ya kukaa hivyo kusababisha usumbufu kwa Watu na usalama wao kwa ujumla.

Pia amesisitiza kuwa kuanzia sasa mifumo ya kupokea wageni wa Kimataifa imeimarishwa kutokea kwenye Uwanja Wa ndege hadi sehemu wanayofikia.


 

Hakuna maoni