Zinazobamba

KAWAIDA ATAKA MABADILIKO NDANI YA UVCCM.

Na Mussa Augustine.

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Mohamed Kawaida amemuagiza Katibu Mkuu Mpya wa Umoja huo Fakii  Lulandala kuhakikisha analete mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Taasisi hiyo.

 Kawaida ametoa agizo hilo leo Oktoba 20, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika hafla ya mapokezi ya Katibu Mkuu huyo  aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt Sama Suluhu Hassan kushika nyadhifa hiyo.

 "Taasisi imepata Mtendaji Mkuu na alishapokelewa na watendaji wenzake Makao Makuu Dodoma na sasa yupo tayari kwa kuanza  kazi za UVCCM, tuna mpango kazi wetu wa miaka mitano na miaka mitatu ambao unapaswa kutekelezwa ipasavyo," amesema Kawaida.

 Nakuongeza kuwa "Tuna Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi iliyojielekeza kuhakikisha tunapambania maslahi ya vijana, hivyo unapaswa kuhakikisha hilo linatimia,".

Aidha Mweyekiti huyo Taifa wa UVCCM  amesema Kama Mtendaji Mkuu wa UVCCM Taifa anapaswa kuhakikisha anawasimamia Watendaji wengine wote katika ngazi mbalimbali ikiwemo wa mikoa na Wilaya ili kufanya Umoja huo uzidi kuimarika kiutendaji nchi nzima.

Aidha amesema Mabadiliko ndani ya UVCCM hataweza kuyafanikisha pasipo na ushirikiano na watendaji wengine, hivyo ametakiwa kushirikiana nao bega kwa bega.

Kawaida amemwagiza pia kuhakikisha Idara ya Chipukizi inakuwa imara kwa kuhakikisha anakuja na mpango wa Wiki ya Chipukizi ambayo Chipukizi wataitumia kuwasilisha changamoto zao na maoni yao kwa maendeleo ya chama.

Kadhalika Kawaida amemtaka Katibu Mkuu huyo kuandaa mpango wa kushugulikia Kero za vijana ambao ni Wakulima, wanafunzi, wajasiriamali, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo na kadhalika ili kupigania maslahi yao na kuwainua kiuchumi.

"Hivyo tushughulike na makundi haya na kushughulikia changamoto zao," ameeleza Kawaida.

Vile vile Kwaida amemuelekeza Katibu Mkuu kuandaa mpango kazi wa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi juu ya vijana. 

Nae Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mengi na makubwa ikiwemo kuwawezesha vijana kwa kiasi kikubwa kwani amewatoa mtaani na kuwapeleka saiti kwenye kilimo, ajira, mikopo kutoka mfuko wa uwezeshaji na kadhalika.

Aidha ameeleza kuwa baada ya miezi minne kupita bila safu ya uongozi wa UVCCM Taifa kukamilika, sasa imekamilika baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu huyo Lulanda


Hakuna maoni