Zinazobamba

GALCO INSURANCE KUTOA HUDUMA YA BIMA YA “TAKAFUL”

Na Mussa Augustine.

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini  (TIRA) Bi.Khadija Said amezitaka wakala zinazotoa huduma za bima kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotolewa na mamlaka hiyo..

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 5,2023 jijini Dar es salaam  wakati wa uzinduzi wa Bima ya TAKAFUL inayotolewa kupitia kampuni ya uwakala ya GALCO Insurance kwa kushirikiana na kampuni mama ya ZIC TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam .

Bi . Khadija amesema kuwa kampuni zote za uwakala wa bima zinapaswa kuzingatia kanunu na sheria zilizowekwa na TIRA  iliwaweze kitoa huduma kwa wateja wao kwa kiwango na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha ameendelea kufafanua kuwa kwa mujibu wa mpango wa kuendeleza sekta ya fedha hadi kufikia mwaka 2030 matumizi ya bima yamelengwa kufikia asilimia 50 lakini mpaka sasa matumizi hayo ni asilimia kumi na tano pekee nakwamba uelewa wa matumizi ya bima umelengwa kufikia asilimia 80 mwaka 2030 ambapo kwa sasa .

Hata hivyo Bi. Khadija amezisisitiza kampuni na wakala za bima kuendelea kutoa elimu kwa watanzania waweze kuchangamkia kujiunga na huduma za bima kwani zinasaidia kutatua changamoto wanazoweza kukumbana nazo wakati wanapokubwa na majanga ya aina mbali mb

"Huduma hii ya Bima ya  Takaful  mchakato wake umeanza rasmi mwaka 2008 kupitia kampuni ya ZIC Insuarance na imezinduliwa  rasmi  miezi mitatu iliyopita na Rais wa  serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein  Mwinyi,hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya Bima ya Misingi ya hesheria ya kislam"TAKIFUL ) lakini huduma hii inatolewa kwa waislam na wakristo kwa ujumla"amesema

Takaful ambayo inasimama kama nguzo katika jamii na inasimama katika misingi ya kushirikiana pale ambapo kutakuwa na majanga au faida.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa makampuni ya GSM  Group yanayomiliki kampuni ya Galco Insuarance Ltd ,Benson Mahenya amesema huduma zao za bima ya Takaful sio sera ila ni ahadi ya kuwa wapo karibu na watu katika kutatua changamoto za kibiashara na kimaisha kiujumla .

"Tunafanya kazi katika misingi ya kweli na uwazi na kuhakikisha usawa katika utoaji wa huduma,tuna uzoefu wa miaka mitano sokoni na katika kipindi hiki tumeweza kutoa huduma kwa watu binafsi zaidi ya mia tano na makampuni zaidi ya kumi ,"amesema Mahenya .

Naye meneja Biashara  Emmanuel Bugabu  amesema kuwa Galco Insurance Brokers inashirikiana na makampuni mbali mbali ya kiwemo MAYZUH COMPAZNY LIMITED ilikutoa mafunzo kwa wafanyakazi  na kuhakikisha wana uelewa na huduma ya Takaful na wanashirikiana na pia na ZIC TAKAFUL LTD katika utoaji huduma hiyo ya bima ya misingi ya kiislam TAKAFUL.

"Nia yetu ni kukuza mwamvuli wetu wa huduma  za bima kwa watu wote wakiwemo mtu mmoja mmoja , wanafamilia,wafanyabiashara na makampuni  au taasisi mbali mbali,nakusisitiza kuwa wafanyakazi wa Galco Insuarance wamepata elimu ya kutosha kutoa huduma kwa wateja" amesema Bugabu.



Hakuna maoni