Dkt Khalid: Daktari wa Mufti wa Tanzania aliyebobea kwenye tiba lishe
Mwandishi wetu, Dodoma
Matatizo ya afya ya akili ni moja ya changamoto kubwa katika
jamii tunayoishi, inaelezwa kuwa ndani ya mwezi mmoja si ajabu kusikia mtu
ameondoa uhai wake au ameondolewa uhai wake kutokana na matatizo ya akili
Utafiti ambao sio rasmi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa
kuna kuongezeka kwa matukio yanayotokana na afya ya akili, kumekuwa na matukio
ya kusikitisha yanayohusisha afya ya akili.
Kule Jijini Mwanza, dada mmoja anayekadiliwa kuwa na miaka 24,
Bi Asteria Wilberd maarufu Mgole akiwa na mtoto wake wa miezi 4 alidaiwa
kupotea, chanzo kikitajwa kuwa ni matatizo ya afya ya akili yaliyo muanza
takribani miezi minne iliyopita
Pia mitaani takwimu ambazo sio rasmi zinaonyesha kumekuwa na
ongezeko la watu wenye changamoto ya afya ya akili, hususani vijana ambao
wamejikita katika michezo ya Kamari na uraibu
Si ajabu siku hizi kumkuta kijana akizungumza peke yake njia nzima, ukibahatika kumuhoji utagundua kuwa changamoto kubwa inayomsumbua ni akili yake kuingiliwa na mambo mengine.
Hakika hakuna jambo baya kama kuharibu akili, utakubaliana na
mimi kuwa akili ni kitu chenye thamani kubwa, ukiondoa thamani ya nafsi kitu
ambacho kinafuata ni akili.
Licha ya umuhimu huo bado kumekuwa watu wanaharibu thamani hiyo
kwa nguvu zote.
Mmoja wa wataalam wa tiba lishe na daktari wa Mufti na Sheikh
Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir, Dkt Khalid Hussein amekili kuwa tatizo
la afya ya akili limezidi kuwa kubwa na kwamba kama hatua stahiki
hazitachukuliwa basi kuna hatari kubwa.
Dkt Khalid ambaye anauzoefu wa tiba lishe kwa Zaidi ya miaka 22
mpaka sasa, amesema maatatizo makubwa ya watu hadi kufikia kuharibu akili zao
ni kuacha kufuata maamlisho ya Mwenyezi Mungu na kuamua kuishi kwa uhuru
wanaoutaka, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeleta hatari na kuharibu akili.
Dkt Khalid ambaye hakusita kueleza ndoto yake ya kutibu wagonjwa
wa uraibu kwa mwezi mmoja kupitia tiba lishe, amesema anajisikia vibaya kuona
watu wanaendelea kuharibu akili ambayo Mwenyezi Mungu amewazawadia. Fuata kiungo hiki kwa faida zaidi kuhusu Dkt huyu
Daktari wa Mufti wa Tanzania aliyebobea kwenye tiba lishe
“Mimi ni Daktari wa tiba lishe, ninafanya tafiti lakini pia ninatatibu magonjwa ambayo tayari nimeyafanyia utafiti, nashukuru Mufti ameona kazi inayofanyika na ameamua kuniteua kuwa daktari wake,” alisema
Pia, Dkt Khalid ambaye ni msomi wa dini kwa ngazi ya thanawi
aliyeipata huko Doha/Qatar amewaomba watanzania kuacha tabia ya kubeza tiba
mbadala akisisitiza kuwa kwa miaka ambayo amefanya kazi ameweza kusaidia watu
wengi na kupona.
“Wapo watu wachache ambao wanabeza tiba asili, lakini nataka
niseme wazi kuwa watu hao elimu bado haijawafikia, hapa nchini kunahatua
zimepigwa ikiwamo baadhi ya hosptali za serikali kuanza kutumia dawa hizi
ikiwamo Hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini Dodoma,” alisema
Akieleza historia yake katika kazi ya utabibu na utafiti wa dawa
lishe, Dkt Khalid amesema ameanza kazi toka mwaka 2001 akiwa nchini Afrika
Kusini katika mji wa Cape town, kitongoji cha Kairisha.
Kisha, alipata fursa ya kuzunguka nchi mbalimbali kufanya tafiti zake ikiwamo Botswana katika mji wa Gaborone, Malawi katika mji wa Lilongwe na Congo katika Mji wa Lubumbashi
Nchi zingine ambazo amefanikiwa kwenda ni pamoja na Visiwa vya
Comoro katika mji wa Moroni, Pemba na Msumbiji katika mji wa Maputo.
“Upande wa elimu sijasoma sana elimu ya sekula zaidi nimejikita
katika masomo ya kiimani, nimesoma sana quran hadi ngazi ya chuo Kikuu,
nimesoma nchini Qatar, Doha huko Falme za Kiarabu,” alisema
Aidha akieleza ilikuaje mpaka akajiunga na fani hiyo, Dkt Khalid
alisema wazo la kutoa huduma hiyo lilikuja baada ya kugundua kuwa kuna wagonjwa
wengi wanateseka kupata tiba ya uhakika kwa baadhi ya maradhi, kwani hospitali
hazina uwezo wa kutibu baadhi ya magonjwa bali wanapunguza makali yake tu.
Ametaja mfano wa maradhi ambayo yanasumbua watu sana lakini
hayana tiba ya uhakika katika hospitali za kawaida ni pamoja na maradhi ya
vidonda vya tumbo na Asma (Pumu).
Pia, Dkt Khalidi ameeleza kufurahishwa kwake kwa kupatiwa nafasi
na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ya kuwa Daktari wake kwani nafasi hiyo ni
nyeti na ameahidi kuisemea tasnia ili wachache ambao bado hawajapata faida ya
kujua thamani ya tiba lishe wapate kuelimika.
“Badhi ya mambo ambayo yamenifurahisha katika kazi yangu ni
kuaminiwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir, kwa kweli sio
jambo dogo, ameniheshmisha katika jamii lakini pia amejibu kwa vitendo kuwa
anathamini kazi zinazofanywa na wasomi wa tiba lishe,” Alisema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni