Zinazobamba

TUZO ZA YOUNG CEO AWARDS ZAZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


NA MWANDISHI WETU

TUZO za Wakurugenzi Vijana (Young CEO Awards) zimezinduliwa leo Septemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Tuzo hizo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Young CEO Roundtable Zakayo Shushu amesema zitashirikisha Vijana wa kiafrika wanaomiliki Kampuni ama Taasisi zinazotambulika nchini mwao.

Shushu amesema lengo la tuzo hizo ni kutambua na kuwatia moyo Vijana kwa kanzi nzuri wanayofanya licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.

“Tunapoona kijana wa kiafrika ameweza kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuzitumia kama fursa, tumeona tuandae mfumo wa kuwapongeza,” amesema Shushu na kuongeza,

“Kwahiyo kwa mwaka huu tuzo hizi zitakuwa ni kwa Afrika nzima na Nchi zaidi ya 50 zitashiriki,”.

Ametaja miongoni mwa faida za kushiriki tuzo hizo ni pamoja na kumpa mshiriki utakbulisho wa Kimataifa, kumuongezea uwezo wa kufanya Biashara Kimataifa na pia zitamjengea kijana uwezo wa kujiamini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ubunifu wa Taasisi hiyo Timotheo Samwel ametaja vigezo vya washiriki kuwa ni pamoja na mshiriki kutambulika katika Nchi yake, umri wake uwe kuanzia miaka 20 hadi 39, kwa Mwenye Kampuni lazima iwe imesajiliwa na kutambuliwa kisheria.

Vigezo vingine ni lazima Kampuni yake iwe imefanya Kazi kwa miaka isiyopungua miwili na awe ameajiri, asiwe ameshitakiwa kwa uvunjifu wa sheria na mshiriki lazima Taasisi au Kampuni yake iwe inatambulika na Watu wengi.


Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo amewatakiwa mafanikio Vijana wote watakaojitokeza kushiriki tuzo hizo.

Hata hivyo ameiomba Serikali na Taasisi za kifedha kuunga mkono juhudi za Vijana.

Hakuna maoni