Zinazobamba

ABOOD AAPA KUWASHUGHULIKIA WALE WATAKAOTAFUNA FEDHA ZA MRADI WA UBORDESHAJI MIJI MOROGORO.

  Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Na Mussa Augustine.

Mbunge wa Morogoro Mjini Abdulazizi Abood amewataka Watendaji wanaosimamia  fedha za miradi ya uboreshaji wa Miundombinu ya Halmashauri za Miji na Manispaa Mkoani Morogoro ambayo imetolewa na Serikali kuisimamia vizuri nakwamba hatakua tayari kuona fedha hizo zinaliwa na wajanja.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 23,9,2023 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika Kwa hafla ya kutiliana saini Mikataba 12 ya awali ya Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania ambapo Mkoa wa Morogoro umetengewa fedha  Dola laki 751,000 sawa na fedha za kitanzania Tsh.Bilioni 19,606,559,115.00 kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya Mkoa wa Morogoro.

Fedha hizo zitatumika katika kuboresha na kujenga  Barabara za kiwango cha  lami,,Masoko ya kisasa,Madaraja ,kuweka taa za barabarani ikiwa lengo ni kuweka miji na Manispaa za Mkoa huo kuweza kukuza uchumi wa Taifa pamoja na mtu mmoja mmoja kutokana na kufanya shughuli za uchumi bila usumbufu.

"Namshukuru sana Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizozifanya za kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha Miundombinu katika Majiji na halmashauri zetu,Mimi kama Mbunge wa Morogoro Mjini nitahakikisha nafuatilia fedha hizi kwa ukaribu kuona kama zimeweza kutumika vizuri katika kutekeleza miradi iliyokusudiwa 'amesema Mbunge Abood.

 

      Mbunge wa Morogoro Mjini Mh.Abdulazizi Abood(Picha na Mtandao)

 Awali akihotubia hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa JNICC jijini Dar salaam Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji yote ambayo yamenufaika na Miradi hiyo kuhakikisha wanasimamia fedha hizo zitumike katika kujenga miradi yenye ubora unaotakiwa nakwamba hatasita kumuondoa Mkurugenzi yeyote ambae ni mzembe.

Waziri huyo wa TAMISEMI amesema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameingia kwenye mioyo ya Watanzania ndio maana anatafuta fedha kwa ajili ya kuboresha Maisha yao hivyo baadhi ya watu ambao watajaribu kukwamaisha jitihada hizo atawachukulia hatua ikiwemo kuwasimamisha kazi.

Waziri Mchengerwa pia amewataka wakandarasi waliopewa zabuni ya kujenga miradi wafanye kazi hiyo kwa weledi na wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba huku akiwataka pia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi hiyo.

" Wakurugenzi wa Majiji,Miji na Halmashauri nawaelekeza mkahakikishe mnasimamia miradi hii ,mjiepushe na vitendo vya rushwa,ubadhilifu wa fedha za miradi,Rais wetu mpendwa ( Dkt Samia Suluhu Hassan) amewaamini ndio akawateua hivyo kamsaidieni raisi kutekeleza miradi hii ambayo tunasaini leo ambapo itashuhusdiwa na  wabunge waliopo hapa" amesema kwa msisitizo Waziri Mchengerwa.

Serikali imepata Dola Milioni 410 bila VAT ikiwa ni Mkopo wa Benki ya Dunia (lDA19) ambapo mradi huo itatekelezwa kwa awamu tatu,ambazo awamu ya kwanza ni Miji 12 katika mwaka huu wa Fedha 2020/2024,kundi la pili ni Miji 15 huku kundi la tatu ni Miji 18 litaanza utekelezaji mwaka wa Fedha 2024 /25  ambapo muda wa utekelezaji utakua miaka sita kuanzia mwaka wa Fedha 2022 / 2023.



Hakuna maoni