DKT. KIJAJI AITAKA NDC KUZALISHA VIUATILIFU VYA VYA KUTOSHA KATIKA MSIMU HUU WA KILIMO
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amekitaka kiwanda Cha Viuatilifu vya kuua mazalia ya Mbu (TBPL) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani kuzalisha bidhaa za Viuatilifu hai kwa ajili ya Msimu huu wa Kilimo kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.
Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo Septemba 21, 2023 wakati akizungumza na Uongozi, Watumishi na Waandishi wa habari baada ya kufanya ziara kiwandani hapo kwa ajili ya kuona utekelezaji wa maagizo ambayo aliyatoa kwa ajili ya uboreshaji wa kiwanda hicho hivi karibuni.
“Nakuongeza kuwa ningependa bidhaa hii Mwezi wa 10 Mwaka huu ianze kuzalishwa kwa wingi na iingie sokoni kwani huu ni msimu wa Kilimo,.
Ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa NDC kwa kutekeleza maagizo aliyotoa alipotembelea kiwanda hicho.
Kwa pande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolas Shombe ameeleza kuwa kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za kibaolojia za kuulia viluwiluwi vya Mbu pamoja na Bidhaa za Mbolea ya Kilimo.
Amesema kuwa kiwanda hicho ni cha kipekee na cha Kimataifa nakwamba pamoja na kuazalisha dawa hiyo ya viluwiluwi wa mbu lakini pia ni maabara kubwa ya bidhaa za kibaolojia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni