TANESCO IMEANZA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA UZALISHAJI WA UMEME JADIDIFU
Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini(TANESCO) limeanza utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Uzalishaji wa umeme jadidifu ili kuongeza mchango wake katika gridi ya Taifa na kuweza kuondokana na changamoto za Nishati hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika Kongamano la tano la kimataifa la maonyesho ya Nishati Naibu Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa shirika hilo Declan Mhaike amebainisha kuwa miradi saba ya umeme jua na Upepo ya Megawati 170 hadi 100.
Amesema miradi hiyo itaongeza mchango wake katika gridi ya Taifa kutoka asilimia 0.5 ya sasa hadi asilimia 20 ifikapo mwaka 2025 nakuwezesha kuwa na umeme wa kutosha.
Aidha Mhaike ameendelea kusema kuwa miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na wa megawati 100 wa upepo iliyopo Makambako Mkoani Njombe, Mradi wa megawati 100 wa Upepo uliyopo Ismani Mkoani Iringa,pia Megawati 60 za Umeme jua uliyopo Dodoma,na Megawati 100 za umeme jua uliyopo Manyoni Mkoani Singida.
Mhaike ameendelea kufafanua kuwa Mradi mwingine unaotarajiwa kutekelezwa ni ule wa Kituo Cha Kishapu Mkoani Shinyanga ambao utazalisha megawati 50 hadi 150 ,huku kuna mradi mwingine utakaotekelezwa Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Awali katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es salaam Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba Serikali imejidhatiti kutekeleza vyanzo vingine vya umeme na sio kutegemea umeme wa Maji pekee na kwamba Tanzania ina mpango wa kua mzalishaji Mkubwa wa Nishati ya Umeme Duniani.
"Lengo letu tunataka tuwe wazalishaji wakubwa wa umeme kupitia rasilimali tulizonazo tuweze kua na umeme wa kutosha ,rahisi lakini pia unapatikana wakati wote,na ikiwezekana tuuze nje ya nchi ,hayo yote yatafikiwa kupitia mjadala huu wa mwelekeo wa namna tunavyoweza kuzalisha" amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ReplyForward |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni