Zinazobamba

TAMPRO YAPATA KATIBU MKUU MPYA, KUBEBA MIKOBA YA SHARIFU

Na Juma Nchia Mfaranyaki-Songea.

Amiri wa Tampro Alhaji Mhandisi Haji Mrisho Lubibi kwa mamlaka aliyopewa na katiba ya Tampro amemteua Ustaadhi Hamza Jafari Mtunu kukaimu nafasi ya katibu mkuu wa Tampro nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Brother Sharifa Mohamed Haji.

Katika taarifa yake kwa ummah Mh Amiri Haji Mrisho amesema uteuzi wa Hamza Mgumu unaanza rasmi tarehe 18 septemba 2023 na kuanza majukumu yake.

Ustaadhi Hamza Mtunu ambaye alikuwa mwanafunzi wa karibu wa mwalimu wa walimu shujaa wa elimu kwa waislam wa Tanzania Almaruhumu Sheikh Buruhani Mtengwa ametoa shukurani zake za dhati kwa viongozi wa Tampro na vyombo vyake vya maamuzi kukubali nafasi hiyo na kuahidi kuitumikia kadri ya uwezo wake ili kuleta tuja kwa ummah.

*"Hakuna namna hili jukumu nimelipokea kwa mikono miwili ,kuwashukuru viongozi wa Tampro na vyombo vyake vya maamuzi kwa kuniteua mimi kwa nafasi hiii,najua ugumu na changamoto za uongozi katika taasisi za wasomi waislamu lakini kwakuwa ni wajibu wetu lazima nikubali,nawaomba wote munipe ushirikiano na muniombee ili Allah anifanyie wepesi katika utekelezaji wa majukumu yangu*"

Amiri Haji Mrisho katika taarifa yake amesema Mh Sharifa Mohamedi aliyekuwa katibu mkuu wa Tampro amepata nafasi nyingine kubwa ya kiutendaji katika shirika kubwa la kimataifa na hivyo analazimika kutumikia nafasi ile bila kuchanganya na majukumu mengine.

*"Tunamshukuru sana kaka yetu Sharifu kwa moyo wake wa kujituma na juhudi kubwa na ubunifu wake muda wote alipokuwa katibu mkuu wetu,tunamtakia kila la heri katika nafasi yake mpya katika shirika kubwa la kimataifa la NAMA na kutokana nafasi hiyo sharti awepo ofisini kimajukumu bila kutumia taasisi zingine kwa nafasi kama hiyo,tutamkumbuka kwa mengi lakini bado tunayo imani kwake kuendelea kuwa mwana Tampro mzuri kama mwanachama kwenye wajibu wake kila la heri kaka Sharifu*"amesema amri Haji Mrisho.

Mh Sharifu Mohamedi ni mtaalamu mshauri wa maswala mbali mbali na amewahi kuwa amiri wa TAMSA TAIFA kabla ya kuwa TAMSYA lakini pia amehudumu kama katibu mtendaji katika taasisi nyingi za kiislamu ikiwemo The Islamic Foundation-TIF ,ALHIDAYA ya Zanzibar na zingine na mchango wake na ufanisi mkubwa kila alipopita hauwezi kusahaulika.

Katika taarifa yake ya kuwaaga wanaTampro Brother Sharifu amesema.

*"Nawashukuru sana WanaTampro kwa dua zenu na ushirikiano wenu kwangu kwa kipindi chote nilichokuwa katibu mkuu wa Tampro,naomba muendelee kunipa ushirikiano kwani majukumu yangu mapya yanahusiana sana na kuiimarisha Tampro na ummah wa kiislamu kwa ujumla.Nampongeza na kumshukuru Kaka yangu Hamza Mtunu kwa kukubali kumpokea jukumu hili naahidi kumpa ushirikiano mkubwa sana wa hali na mali katika kufanikisha majukumu yake,nitaendelea kuwa Tampro na nitatimiza wajibu wote kama "active member"*.Amesema Sharifu

Tampro ni moja ya jumuiya ya kipekee ya waislamu inayozingatia na kufuata utaratibu katika kuchagua na kuteua viongozi wake kwa mujibu wa sifa za taasisi na mtu anaeteuliwa kushika majukumu ya Tampro, jambo ambalo inaifanya Tampro kuwa taasisi bora tofauti na taasisi zingine.

*Wasifu wa kaimu katibu mteule Mh Ustaadhi Hamza Mtunu umebainshwa wazi katika andiko la wasifu wake yaani 'CV' ambalo utaletewwa hivi punde lakini kwa faida ya wasomaji wa makala hii*

Mh Hamza Ntunu ni msomi wa kiwango cha shahada ya uzamili shahada ya pili Masters na mlolongo wa astashahada mbali mbali za masomo ya muda mfupi na muda mrefu kutoka vyuo vikuu tofauti hapa nchini.

*Mh Hamza Mtunu mzoefu na mbobezi katika kufanya utafiti na ushauri wa kitaalamu ,kutoa mafunzo na masuala yote ya uongozi.*

Kwa sasa ni mkurugenzi mwenza wa kampuni ya BLUE BELT BUSINESS ASSOCIATE LIMITED kampuni inayofanywa kazi mikoa Kwanza,Dodoma,Arusha,Morogoro,Mtwars na Tanga.

*Licha ya majukumu hayo mazito katika kampuni yake bado amekubali wito wa kuwatumikia waislamu kupitia nafasi hiyo ya kukaimu ukatibu mkuu wa Tampro jambo* *ambalo sio rahisi sana kwa wasomi waislamu kukubali majukumu hata kama hana jukumu* *lingine au anao muda wa kutosha kutekeleza majukumu*

*ya Tampro kwa hakika Mh Mtunu anastahili pongezi*

Wasomi mbalimbali na viongozi wa kiislamu wametoa pongezi za dhati kwa Mh Mtunu kwa uteuzi huo,Mh Dr Pazi Mwnyinvua Semili ambaye ni katika waasisi wa Tampro na ameshika nafasi mbalimbali ikiwemo ukatibu mkuu kwa awamu zaidi ya moja lakini sasa Dr Pazi ni katibu wa baraza la wazee wa Tampro amesema...

*"Kwa niaba ya wazee wa Tampro tunampongeza Mh Amiri Haji Mrisho kwa juhudi zake za kushughulikia changamoto za Tampro lakini tuna karibisha na kumpongeza mtaalamu wetu Mh Mtunu ,wazee wa Tampro tunaimani kubwa na uteuzi wake tunaamini hatawaangusha waislamu,aidha nitumie fursa hii pia kumpongeza na kumshukuru Brother Sharifa kwa utumishi wake uliotukuka ndani ya Tampro,tunawasihi viongozi wa taasisi na jumuiya zote za kiislamu kubwa na nia njema katika kubadilishana madaraka kama walivyofanya vijana wetu hawa Brother Sharifu Mohammedi na Mh Hamza mtunu kwani taasisi nyingi viongozi hawakabidhiani na hawashirikiani matokeo yake wanaokuja wanaanza upya na waliokuwepo wamezama na nyaraka zote na huo ndiyo mwanzo wa upotevu wa mali za waislamu,tunamtakia kila la heri Mh Mtunu katika majukumu yake na kila la heri Brother Sharifu.*"Amehitimisha Dr Pazi.

Wanatampro sehemu mbalimbali wamempongeza Mh Hamza Mtunu na kumuombea afya njema katika majukumu yake huku wakionesha matumaini makubwa katika kuipeleka mbele Tampro.

Mh Yusufu Ugutu ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TANZANIA CENTER FOR EDUCATION ambayo kwa sasa unatambulika kama mkombozi wa elimu Zanzibar ametoa maoni yake moja kwa moja akiwa visiwani humo kwenye semina za walimu wa darasa la nne Mh Ugutu Amesema...

*"Licha ya kumpongeza Mh Mtunu n kumtakia afya njema ,muhimu pia ajue kiu na matarajio ya wana Tampro yapo wapi ili yeye atusaidie kuyatekeleza kwa kututuma na kutuagiza tupo tayari kumsaidia,pamoja na kazi nzuri walizofanya viongozi waliotangulia tuna imani Mh Mtunu ataongeza speed katika mambo yafuatayo......*

1.Mawasiliano thabiti baina ya ofisi yake na clinic zotena matawi yote kuongeza uhai na uwajibikaji.

3.Uanzishwaji wa program za kusaidia vijana kufaulu mitihani na kuondoa division zero kwa vijana wa kiislamu.

4.Vikao vya Tampro na taasisi na jumuiya za kiislamu ili kuwa na kauli moja katika mambo ya kitaifa 

5.Kuongeza speed wanachama kutoka michango yao ya mwezi lakini wapo wenye uwezo mkubwa sana kifedha nao wanatoa kumikumi kama wengine kwa mwezi ni vizuri kukawepo utaratibu wa maelewano wengine watoe michango yao kulingana na kipato chao.

5.Ujenzi wa jengo la TAMPRO HOUSE uende speedi kwani tayari jengo letu limezungukwa na mijengo mikubwa sana kama vile kwa mbele yake soko la magomeni,ubavuni mwake ofisi ya manispaa ya kinondoni.*jengo letu kuonekana kama kituko vile lilivyo kwa hiyo tunaamini uteuzi wake utaongeza chachu ya kukamilika jengo hilo kwa haraka. Ni hayo tu Uncle J wasalimie huko bara.*...Amehitimisha Brother Yusufu Ugutu

           ...........

*iBrand Tanzania 🇹🇿🎤 inatoa pongezi nyingi sana kwa kaimu katibu Mteule na inamtakia kila la heri katika majukumu yake,zaidi tunamuahidi ushirikiano wa hali na mali muda wote.*

..................................

Imeandikwa na 

Juma Nchia 

Mratibu wa Matawi Tampro-Taifa.

Safarini Songea.

Juma-nne saa 9:00 usiku.

0784822332.🙏🏽

*Ni Ustaadhi Hamza Jafari Mtunu*

*Ni mbobezi katika tafiti,ushauri,mafunzo uongozi*

          ..............

Na Juma Nchia 

Mfaranyaki-Songea.

          ...............

Hakuna maoni