Zinazobamba

TABIBU MADUHU: NYASOSI TRADITIONAL CLINIC TUNATIBU MAGONJWA YA PRESHA NA SUKARI.

Magonjwa ya Shinikizo la Damu(PRESHA) pamoja na Sukari yamekua tishio kubwa duniani kote nakuchangia kuwepo kwa ongezeko la  vifo vitokanavyo na Magonjwa hayo..

Hali hiyo imesababisha Wataalamu mbalimbali wakiwemo wa tiba za Asili kufanya tafiti  mbalimbali  zitakazosaidia kupatikana kwa dawa ya kutibu Magonjwa hayo.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Tabibu Emmanueli Maduhu ambaye ni Mkurygenzi Mkuu wa Kituo cha utafiti na utoaji wa huduma za matibabu ya Asili na Ushauri cha Nyasosi Traditional Clinic kilichopo Magomeni Kanisani Jijini Dar es salaam amesema kuwa Magonjwa hayo kwa sasa ni tishio kutokana na kuwakumba vijana na Watu wenye Umri Mkubwa.

Ugonjwa wa Presha.

Tabibu Maduhu anasema kuwa ugonjwa huo unazidi kukua kila siku 

Aidha amesema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na Sababu mbalimbali ikiwemo Msongop wa Mawazo unaochangiwa na sababu mbalimbalikama vile mtu kupatwa na malazi.

"Sisi Kama Nyasosi tuna dawa ambazo zinarudisha mzunguko wa damu kua wa kawaida pia tunatoa ushauri na maelekezo namna ya kuepukana na Ugonjwa huu".amesema Tabibu Maduhu.

Amendlea kufafanua kuwa Jamii lazima ijifunze kula vyakula ambavyo havileti madhara katika afya zao ikiwemo kuepuka kula vyakula vya mafuta mengi kwani vinaharibu mzunguko mzuri wa damu.

Ugonjwa wa Sukari.

Tabibu Maduhu anasema kuwa ugonjwa huo umekua tishio duniani kote hadi inafikia wakati wataalamu wanasema hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huo.

Anasema kuwa kituo chake kimefanya utafiti kwa muda wa miaka minane  nakupata dawa ambayo ni suluhisho la ugonjwa huo,huku akisema kuwa chanzo cha ugonjwa huu ni kua na sukari nyingi kwenye damu.

"Kuna Sukari ya kurithi na Sukari ya kuipata kutokana na mtindo mbaya wa maisha yaani ulaji mbovu wa vyakula na vinywaji,hivyo chanzo chake ni kongosho kushindwa kuzalisha insulini ya kutosha kwa ajili ya kusaga sukari iliyopo kwenye damu ndipo mtu anaugua ugonjwa wa sukari"amesema.

Tabibu Maduhu amezitaja dalili za ugonjwa huo kua ni pamoja na kupata haja ndogo kila wakati nyakati za Usiku na Mchana ,mwili kuchoka ,kuhisi njaa na kinga za mwili kushuka lakini pia mwanaume au mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Amefafanua kua chanzo cha kongosho kushindwa kuzalisha insulini nikutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Malaziya figo,Moyo,Mapafu,Presha na Mitindo ya Maisha(Ulaji wa Vyakula vya Mafuta mengi na nyama Nyekundu) ,Unywaji pombe,uvutaji wa sigara ,Saratani.

"Nyasosi Traditional Clinic tumefanya utafiti kwa miaka minane hivyo wenye magonjwa hayo Waje wapate matibabu ya aina mbili ,mosi wapate dawa za kutibu ugonjwa lakini pili wapate ushauri wa namna ya kutumia vyakula na vinywaji ambavyo havitaleta madhara yakiafya."amesema.

Nyasosi Traditional Clinic ni kituo ambacho kinafanya utafiti wa magonjwa mbalimbali ambayo  ni Sugu na utoaji wa huduma za matibabu ya asili kwa mujibu wa sheria. 


Hakuna maoni