DIWANI LYOTO AOMBA USHIRIKIANO KWA WANANCHI MZIMUNI KULETA MAENDELEO.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto
Na Mussa Augustine.
Diwani wa
Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam Manfred Lyoto amewaomba Wananchi wa Kata
hiyo kuendelea kushirikiana katika kupambana na Maadui watatu ambao ni
Umasikini,Malazi na Ujinga.
Diwani Lyoto
ametoa wito huo Agost 31,2023 wakati akizungumza na Mwandishi wa habari
hizi ambapo amesema kwamba lengo kuu la uongozi wake ni kuhakikisha
kata ya Mzimuni imepiga hatua kubwa katika shughuli za maendeleo.
“Tumeanzisha
taasisi ya kutoa mikopo isiyo na riba ili Wananchi wajikwamue kiuchumi kwa
kupata mikopo na kuanzisha biashara lakini tumebadilisha utaratibu umekua
Selective kwasababu wengi wao tumegundua wanataka kuchukua mikopo lakini hawapo
tayari kurejesha mikopo hiyo” amesema Diwani Lyoto.
Nakuongeza “tumejifunza
kupitia mikopo ya asilimia kumi iliyokua ikitolewa na Halmashauri ambapo mpaka
sasa ni takribani Bilioni nne au tano hazijarejeshwa jambo ambalo Wananchi
wanaikatisha tamaa serikali ambayo ilikua na nia njema ya kuwasaidia Wananchi
Kiuchumi.
Aidha
amesema kuwa Mikopo hiyo ililenga kuondoa Umasikini na kuwafanya wananchi kupata
maendeleo yenye uhakika wa kupata huduma bora za kimaisha kama vile Chakula na Malazi ,lakini wananchi
wengi wanaokopa hawarudishi mikopo hiyo kwa wakati.
Akizungumzia kuhusu Mmomonyoko wa maadili kwa Vijana amesema kuwa wanajifunza tabia mbaya kama vile Usagaji kutokana na Umasikini kwani wazazi wengi wanaishi chumba kumoja na watoto wao na inapotokea wazazi hao wanafanaya tendo la ndoa unakuta watoto wanangalia hivyo nao wanaenda kufanya majaribio kwa vitendo.
“Kama Wazazi
tunapaswa kuja na jibu maalumu la kutatua nchangamoto ya tatizo la umasikini
ili wazazi wawe na uwezo wa kuisha kwenye nyumba inayojitoshereza kulingana na
ukubwa wa familia”amesema
Diwani Lyoto
amesema Chanzo kingine na stori za mtaani ambazo zinazungumzwa na Watu wakiwa
vijiweni hivyo watoto wanajifunza na wao wanakumbwa katika kadhia hiyo.
“Zamani Mtu
akiwa na umri mkubwa ni ishara yakua na busara kwenye jamii lakini sasahivi
hakuna busara,unakuta jitu zima tena lizee kabisa halijiheshimu na badala yake
linazungumza manene machafu” amesema.
Akizungumzia masuala mengine ya maendeleo katika kata ya Mzimuni Diwani huyo amesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara hivi karibu kwa ajili ya kuwaelezea wananchi pamoja na kukabidhi Vifaa vya michezo kwa timu kumi kwa ajili ya kuendeleza soka katani humo nakuinua vipaji vya vijana.
“Nimeshafanaya
mazungumzo China ili kupeleka vijana kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa ,tatizo vijana wengi ni wavivu na hili ni janga la Taifa lazima
tushirikiane vijana waache uvivu”amesema
Pia
ameongeza kuwa “natarajia kutoa bima za afya kwa wazee wapatao mia moja ili
kuwawezesha kupata huduma za matibabu bure ,hivyo tuna mambo mengi yakufanya
yakimaendeleo naomba wananchi tushirikiane kwa pamoja.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni