Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji
Na Mussa Augustine.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dkt Ashatu Kijaji amewataka wawekezaji Wazawa ambao wamepewa zabuni ya
kuchimba Makaa ya Mawe katika mradi wa Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Njombe
kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Serikali ya uendelezaji
wa miradi ya Kimkakati..
Waziri Dkt Ashatu amesema
hayo Septemba 12,2023 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya utiaji
saini wa Mikataba ya makubaliano kati ya Makampuni matano ya Wazawa na Shirika
la Taifa la Maendeleo( NDC) ambayo yatatekeleza mradi wa Liganga na Mchuchuma
kwakua ni maendelezo ya maono ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendeleza sekta
ya Viwanda na Biashara hapa nchini.
" Hii ni dhamira
ya dhati naya hali ya juu ya serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha ndoto za
utekelezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma sasa zinatimia na rasilimali hizi
ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kuwanufaisha wananchi ziwanufaishe na
kuchangia katika uchumi wa nchi" amesema Dkt Ashatu
Aidha amesema kwamba
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tayari ameridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni
15.4 ikiwa ni malipo ya fidia kwa wananchi wapatao 1142 ambao watapisha
utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza kwa kufanyika utafiti
mapema mwezi huu.
Wananchi 1142
wanatarajiwa kulipwa fidia,kati yao 1118 tayari wamelipwa fidia ,24 bado na
kati yao 19 bado hawajulikani ,huku 5 wanakamilisha ili walipwe fidia zao,hivyo
hawa 19 ambao hawajulikani mradi utakapoanza hawaonekani basi tutasitisha
malipo yao" amesisitiza Waziri huyo wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu.
Dkt Ashatu amesema
kwamba kwa nyakati tofauti Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akisema
ni wakati sasa umefika kwa rasilimali iliyopo katika miradi ya kimkakati ya
Liganga na Mchuchuma kuanza uzalishaji na kwamba ni shauku yake kuona mradi huo
wa muda mrefu unatekelezwa.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa shirika la Taifa la Maendeleo ( NDC) Dkt Nocolaus Shombe
Awali akizungumza Mkurugenzi Mwendeshaji wa shirika la Taifa la
Maendeleo ( NDC) Dkt Nocolaus Shombe amesema kuwa awali mchakato huo ulihusisha
jumla ya Kampuni ishirini na tano (25) ambapo jumla ya kampuni kumi na saba(
17) zilifanikiwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya uchambuzi na ushindani na
hatimaye zilipatikana kampuni tano zilizokidhi vigezo.
" Kampuni
ishirini na tano ( 25) zilipewa nyaraka za zabuni kupitia mfumo wa ununuzi
serikalini ( TANePS) ambapo kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za
zabuni,nakwamba kila kampuni itazalisha tani 30 kila mwezi sawa na tani 150 kwa
kampuni zote tano kwa mwezi " amesema Mkurigenzi huyo Mwendeshaji wa NDC
Dkt Shombe.
Dkt Shombe ameendelea
kusema kuwa mradi huo utakua na manufaa makubwa kiuchumi ikiwemo kutoa ajira
zaidi ya mia tano za moja kwa moja ,ikirahisisha upatikanaji wa nishati
inayotokana na makaa ya mawe kwa Viwanda hali ambayo itachochea ukuaji wa
viwanda nchini pamoja na kuingiza fedha za kigeni kwa mkaa utakaouzwa nje ya
nchi hususani nchi za jirani.
Jumla ya kampuni tano
zimetia saini makubaliano hayo ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika mradi wa Mchuchuma
ambazo ni Sheby Mix Investment Limited ,Nipo Engineering Company Limited,Chusa
Mining Company Limited ,Kindaini Company Limited na Cleveland Mine and Service
Company Limited ,mkataba ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano.
Akizungumza kwa niaba
ya Makampuni hayo Ndaisaba Ruhoro ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya
Cleveland Mine and Service Company Limited ameihakikishia serikali kuwa
watafanya kazi kwa weledi mkubwa huku wakiipongeza serikali ya awamu ya Sita
kwa kuweza kuwathamini na kuwaamini watanzania katika kuwekeza kwenye
miradi mbalimbali hapa nchini.
" Kwa niaba ya
wenzangu napenda kulishukuru shirika la Taifa la Maendeleleo ( NDC) Wizara ya
Viwanda na Biashara na Serikali kwa ujumla kwa kutupa nafasi hii baada ya
kukidhi vigezo mlivyoweka,tunamhakikishia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa
tutafanya kazi nzuri kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia makubaliano ya
kimkataba" amesema Ruhoro.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni