Zinazobamba

Wajiki wanavyokemea rushwa ya ngono kwenye vyombo vya moto

 TAASISI ya Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI) imewaomba madereva wa vyombo vya moto kupinga rushwa ya ngono kwa vitendo ikiwemo kuacha kuwatania wanafunzi kwa kuwaita Majina kama mchumba, mke wangu, mrembo, mchuchu na king'asti. 

Aidha  Diwani wa Kata ya Charambe, Twahir Kamona naye ameungana na Wajiki kutoa wito kwa jamii kuwalnda watoto huku akiahidi kutumia nafasi yake kushawishi wakubwa itungwe Sheria ya kuzuia matumizi ya maneno tata  yakiwemo mchumba na mke wangu ambayo yanayoashiria kuwarubuni watoto na kujiingiza katika ngono. 

Rai hiyo imetolewa hivi  katika kampeni ya mafunzo kuhusu mbinu, vyanzo na madhara ya rushwa ya ngono katika vyombo vya usafiri iliyofanyika katika Kituo cha Mabasi na Daladala cha Mbagala. 

Wajiki imekuwa ikiendesha kampeni dhidi ya rushwa ya ngono katika vyombo vya usafiri inayowaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike hasa wanafunzi.

Katika kampeni hiyo ya Safiri Salama Bila Rushwa ya Ngono inayofanyika katika vituo mbalimbali vya daladala, bajaji, bodaboda, malori na katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nkoani Dar es Salaam, inayofadhiliwa na Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WTF-T), Wajiki imekuwa ikisisitiza jamii kuungana kuhakikisha watoto na wanafunzi wa kike wanakuwa salama waendapo au kutoka shuleni.

Walisema ili kufanikinisha azima hiyo, nguvu ya pamoja ya jamii inahitajika.

Kwa mujibu wa Mongomongo, vita dhidi ya rushwa ya ngono inakwamishwa na uwepo wa usiri na ukimya,  ukosefu wa taarifa na takwimu sahihi za kutosha, kuwapo mikakati dhaifu ya kuikabili na uelewa mdogo wa jamii kuhusu maana, mbinu na madhara ya rushwa ya ngono.

“Rushwa ya ngono katika vyombo vya usafiri inawafanya watoto wetu kuingia katika matatizo ya kupata mimba za utotoni, magonjwa ya kuambukizwea kama ukimwi, kuathirika kisaikolojia na kushindwa kufikia ndoto na malengo yao,” alisema Moingomongo.

Diwani Kamona aliyekuwa mgeni rasmi alisema wakati wa ufunguzi kuwa, umefika wakati viongozi wakiwamo watunga sera kujadili na kupitisha msimamo juu ya mazingira na wakati au umri unaoruhusiwa kwa mtoto kuitwa mchumba, mrembo, mke na kusifiwa kupendekza kwani maneno hayo yanachangia vitendo vya ubakaji kwa kupitia rushwa ya ngono kwa watoto.

Awali katika ujumbe kwa nyimbo, watoto walisema miongoni mwa maneno yanayotumiwa na wahusika wa rushwa ya ngono wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri au mtaani ni kuwaita mchumba, mke, mrembo, na kusifiwa kupendeza.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Kusini mwa Tanzania (Umakuta), Mwishehe Chambuso alisema madereva na makondakta wanapaswa kuwa waadilifu na washirika wa ulinzi na usalama wa watotoi nyumbani na katika vyombo vya usafiri wanavyofanyia kazi.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Mbagala, Mecky Mwingira aliilamu tabia ya baadhi ya wazazi kutokuwa karibu na michezo ya watoto.

Hakuna maoni