JUKATA LIMEIOMBA SERIKALI KUACHANA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA KATIBA MPYA KWA MIAKA MITATU.
Jukwaa la
Katiba Tanzania JUKATA limeiomba Serikali kuanchana na Mpango wa kutoa Elimu ya
Katiba ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu kama ilivyotoa msimamo huo kupitia
aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbalo badala yake ipeleke
miswada ya Sheria za michakato wa katiba Bungeni kwa ajili ya marekebisho.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari leo Agost 31,2023 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa (JUKATA) Bob
Chacha Wangwe amesema ni vyema serikali kuona umuhimu wa kutumia nyaraka muhimu
za mchakato wa katiba Mpya katika kutunga au kurekebisha Sheria za mchakato wa
katiba kwakuwa zimezingatia mahitaji ya sasa ya nchi pamoja uzoefu wa mchakato
uliokwama mwaka 2014.
"Tunatoa wito kwa Waziri wa katiba na Sheria Balozi Pindi Chana kutoa mapema ratiba za hatua za mchakato wa katiba mpya ili kuondoa sintofahamu ambayo imetawala miongoni mwa Watanzania kwa ujumla " amesema Wangwe
Ameendelea kufafanua kuwa JUKATA bado inaamini hatua iliyotangazwa na wizara ya Katiba na Sheria hivi karibuni ya kutoa Elimu ya katiba kwa miaka mitatu ni hatua ambayo inatakiwa kuangaliwa upya kwani ni ucheleweshwaji wa kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kutumia vibaya fedha za watanzania kwani hatua hiyo ilishafanyaika na iliyokuwa tume ya marekebisho ya katiba.
" Ujio
wa Balozi Dkt Pindi Chana katika Wizara ya Katiba na Sheria tunaamini
utaleta nuru ya upatikanaji wa katiba na kuondoa vikwazo ambavyo kwa namna Moja
ama nyingine vitaweza kutukwamisha kama hilo la kutoa elimu ya Katiba ya mwaka
1977 kwa miaka mitatu " amesema
Awali
akizungumza Mwenyekiti wa JUKATA Dkt Ananillea Nkya amesema Mchakato wa
upatikanaji katiba mpya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutengeneza
Sheria mfano ambayo itawafanya watanzania wote wajue namna ya kupata katiba mpya
.
Dkt Nkya
amewasihi watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kupata katiba mpya kwakuwa
jambo hilo halihitaji kuwa na utashi wa kisiasa hivyo linahitaji Uzalendo wa maslahi mapana ya kitaifa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni