Mwalongo awaasa watanzania kutunza mazingira, awakaribisha mnazi mmoja, ni katika wiki ya tiba asili ya Mwafrika
Katibu wa shirika
la dawa asili na utunzaji wa mazingira Boniventure Mwalongo amewataka
watanzania kutunza mazingira na kuacha tabia ya kukata miti hovyo kwani miti ya
asili ina faida nyingi kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumza na
wanahabari bwana Boniventure Mwalongo amebainisha kuwa kupitia miti ya
asili watanzania tumepata faida nyingi ikiwepo kipindi cha covid 19 watu
walitibiwa kupitia miti na mimea ya asili kwani miti mingi hapa nchini
inatumika kama tiba .
Bwana Mwalongo
ametoa wito kwa wadau wa mazingira na tiba asili kujitokeza kwa wingi katika
kongamano la wadau wa mazingira na tiba asili kujitokeza kwa wingi katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 27 mpaka 31 ambapo
elimu mbalimbali za tiba za kisuna na tiba asili na mazingira watanufaika.
Aidha katibu huyo
amefafanua kuwa kupitia mimea na miti ya asili watoa huduma watapata elimu
kwani mpaka sasa wamekuwa wakitoa huduma ya kutengeneza dawa kupitia miti ya
asili kwa wagonjwa waliopo katika hospitali za serikali magonjwa kama
kansa,covid 19,kisukari,afya ya akili wamepata nafuu kupitia dawa hizo.
Kongamano hilo la
wiki ya maadhimisho hayo linatarajiwa kuwa na waratibu wa tiba hizo kutoka
halmashauri 184 za nchi ya Tanzania,mikoa 26 ya Tanzania bara,vyuo kama Nelsoni
Mandela,chuo kikuu cha Dar es salaam,Sokoine,ITN,Nimri na vyuo vingine ambapo
pia kutakuwa na mijadalq ya kisayansi inayohusu mchango wa miti ya asili na
ufanisi wake na namna ya kwenda kwenye majaribio ya kisayansi.
Aidha maadhimisho
hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa katibu mkuu wizara ya afya ambapo wizara wa
afya ndio wasimamizi wakuu wa maadhimisho hayo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni