Uchambuzi matokeo ya somo la dini EDK kwa mwaka 2023 huu hapa, shule zinazoshiriki zaongezeka, wanafunzi 16,000 washindwa kufanya mtihani
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU ULIOFANYIKA TAREHE 09.08.2023
1.0. Utangulizi
Islamic Education
Panel inatangaza matokeo
ya mtihani wa darasa la saba wa Elimu
ya Dini ya Kiislamu na lugha ya kiarabu uliofanyika August 9, 2023 pamoja na mtihani wa kuhitimu madrasa uliofanyika
August 12 na 13, 2023.
Jumla ya shule 3975 katika mikoa 26 ya Tanzania bara na
visiwa viwili (02) vya Zanzibar (Unguja na Pemba) zimeshiriki mtihani huu.
Halmashauri 159 zilishiriki kufanya mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya
Kiislamu.
2.0.Mahudhurio ya watahiniwa
Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa
somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu walikuwa 174,719. Watahiniwa waliofanya mtihani
ni 157,823 sawa na asilimia 90.33. Idadi ya watahiniwa ambao hawakufanya mtihani
kutokana na sababu mbalimbali ni 16,896 sawa na 9.67%.
2.1. Jedwali linaloonesha ulinganisho wa takwimu za
watahiniwa waliofanya mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu mwaka 2022
na mwaka 2023.
MWAKA |
MIKOA |
HALMASHAURI |
IDADI YA
SHULE |
IDADI YA WATAHINIWA |
2022 |
25 |
151 |
3903 |
150,945 |
2023 |
28 |
159 |
3975 |
157,823 |
ONGEZEKO(IDADI) |
3 |
8 |
72 |
6878 |
ASILIMIA YA ONGEZEKO (%) |
12 |
5.3 |
1.8 |
4.56 |
2.2 Idadi ya
Halmashauri zilizoshiriki katika mtihani huo imeongezeka kwa Halmashauri 8
kutoka Halmashauri 151 mwaka 2022 hadi kufikia halmashauri 159 mwaka 2023 sawa
na asilimia 5.3
2.3
Idadi ya shule zilizofanya imeongezeka kutoka
3,903 mwaka 2022 hadi 3975 mwaka 2023 ambayo ni sawa na ongezeko
asilimia 1.8
2.4 Idadi ya
watahiniwa waliofanya mtihani imeongezeka kwa watahiniwa 6878 sawa na asilimia
4.56 kutoka watahiniwa 150,945 mwaka 2022 hadi watahiniwa 157,823 mwaka 2023.
3.0.
Ufaulu
Mtihani
ulikuwa na jumla ya alama hamsini. Matokeo yametolewa kwa madraja A hadi
E. Mtahiniwa
anahesabika kuwa amefaulu ikiwa amepata daraja A, B, C au D.
3.1 Idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi D ni
139,181 sawa na asilmia 88.19 ya watahiniwa wote 157,823. Idadi ya watahiniwa
waliopata daraja E ni 18,591 sawa na asilimia 11.81 ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani.
Idadi ya
watahiniwa na madaraja yao ni kama inavyoonyeshwa katika Jeduali hapa chini:
3.1 Jedwali linaloonyesha ufaulu
wa watahiniwa kwa mgawanyo wa madaraja
DARAJA |
A |
B |
C |
D |
E |
IDADI |
2,681 |
8,663 |
48,037 |
79,803 |
18,591 |
ASILIMIA |
1.70 |
5.49 |
30.44 |
50.56 |
11.78 |
3.2
Shule kumi
bora kitaifa katika kundi la shule zenye watahiniwa 20 au zaidi. Shule kumi
bora zenye watahiniwa 20 au zaidi zimepangwa kuanzia shule yenye ufaulu wa juu
kabisa kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapa
chini.
3.3
Jedwali linaloonyesha shule kumi bora katika kundi la
shule zenye watahiniwa 20 au zaidi.
S/N |
JINA LA
SHULE |
HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
MBAGALA ISLAMIC PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA TEMEKE |
DAR ES SALAAM |
49.33 |
2 |
MUZDALIFA ISLAMIC PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA NACHINGWEA |
LINDI |
49.08 |
3 |
IBUN JAZAR PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA MKURANGA |
PWANI |
48.48 |
4 |
MUMTAAZ PRIMARY SCHOOL |
JIJI LA MWANZA |
MWANZA |
46.77 |
5 |
BISMARCK PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA ILEMELA |
MWANZA |
46.65 |
6 |
RAHMA PRIMARY SCHOOL |
JIJI LA DODOMA |
DODOMA |
46.62 |
7 |
KANGA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA MAFIA |
PWANI |
46.03 |
8 |
ALGEBRA ISLAMIC PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA KIGAMBONI |
DAR ES SALAAM |
46.03 |
9 |
KYENGE ISLAMIC PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA BUKOBA |
KAGERA |
45.88 |
10 |
MUZDALIFA PRIMARY SCHOOL |
MJI WA MASASI |
MTWARA |
45.71 |
3.4 Shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 20.
Shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa
chini ya 20 zimepangwa kuanzia shule yenye ufaulu wa juu kabisa kama
inavyoonyeshwa katika jedwali hapa
chini.
3.5 Jedwali linaloonyesha shule
kumi bora zenye watahiniwa chini ya 20
S/N |
JINA LA
SHULE |
HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
AL-BAYAAN PRIMARY SCHOOL |
ILALA |
DAR ES SALAAM |
46.72 |
2 |
KINYELEZI ISLAMIC PRIMARY SCHOOL |
ILALA |
DAR ES SALAAM |
46.63 |
3 |
ZASHAZ PRIMARY SCHOOL |
ARUSHA JIJI |
ARUSHA |
45.2 |
4 |
KAHAMA PRIMARY SCHOOL |
KIBONDO |
KIGOMA |
45 |
5 |
MALEMBO PRIMARY SCHOOL |
NGORONGORO |
ARUSHA |
45 |
6 |
ALHIJRA PRIMARY SCHOOL |
HAI |
KILIMANJARO |
44 |
7 |
SENGEREMA MUSLIM PRIMARY SCHOOL |
SENGEREMA |
MWANZA |
43.81 |
8 |
LOLIONDO PRIMARY SCHOOL |
NGORONGORO |
ARUSHA |
43 |
9 |
HIDAYA MEMORIAL PRIMARY SCHOOL |
LINDI MANISPAA |
LINDI |
43 |
10 |
AL- RAHMAH PRIMARY SCHOOL |
MKURANGA |
PWANI |
42.78 |
3.6
Shule kumi
za mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa 20 au zaidi. Shule kumi
za mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa 20 au zaidi zimepangwa kuanzia
shule yenye ufaulu mdogo kabisa kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapa chini.
3.7
Jedwali linaloonyesha shule kumi za mwisho katika
kundi la shule zenye watahiniwa 20 au zaidi.
S/N |
JINA LA SHULE |
HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
MISHA PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA TABORA |
TABORA |
5.85 |
2 |
IZENGA PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA TABORA |
TABORA |
6.46 |
3 |
MAKOKANE PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA SAME |
KILIMANJARO |
6.64 |
4 |
YELAYELA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA URAMBO |
TABORA |
6.9 |
5 |
KISHAA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA SAME |
KILIMANJARO |
7.61 |
6 |
YOMBOLUKINGA |
WILAYA YA KISARAWE |
PWANI |
7.63 |
7 |
IGAMBILO PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA TABORA |
TABORA |
7.64 |
8 |
SONGAMBELE PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA URAMBO |
TABORA |
7.67 |
9 |
MAJENGO PRIMARY SCHOOL |
MJI WA MPANDA |
KATAVI |
7.71 |
10 |
UYUI PRIMARY SCHOOL |
MANISPAA YA TABORA |
TABORA |
7.79 |
3.8 Shule kumi za mwisho kitaifa katika kundi la shule
zenye watahiniwa chini ya 20.
Shule kumi za mwisho katika
kundi la shule
zenye watahiniwa chini
ya 20 zimepangwa kuanzia shule yenye ufaulu mdogo kabisa kama
inavyoonyeshwa katika jedwali hapa chini.
3.9
Jedwali linaloonyesha shule kumi za mwisho katika
kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 20
S/N |
JINA LA
SHULE |
HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
ANTSA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA KARATU |
ARUSHA |
3.33 |
2 |
NSIMBO PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA NSIMBO |
KATAVI |
3.67 |
3 |
KWAUGORO PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA MERU |
ARUSHA |
4 |
4 |
CHEMCHEM PRIMARY SCHOOL |
MJI WA BABATI |
MANYARA |
4.5 |
5 |
NAMBEHE PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA NAMTUMBO |
RUVUMA |
5 |
6 |
MVUNGWE PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA SAME |
KILIMANJARO |
5 |
7 |
NYAMTENGELA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA USHETU |
SHINYANGA |
5 |
8 |
NKWAMAKUU PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA HAI |
KILIMANJARO |
5 |
9 |
SARJANDA PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA HANANG |
MANYARA |
5 |
10 |
IGUMO PRIMARY SCHOOL |
WILAYA YA IGUNGA |
TABORA |
5 |
3.10
Halmashauri kumi (10) bora.
Halmashauri kumi bora
zimepangwa kuanzia halmashauri yenye ufaulu wa juu kabisa kama zinavyoonyeshwa katika
jedwali hapa chini.
3.11 Jedwali linaloonyesha Halmashauri kumi (10) bora.
S/N |
JINA LA
HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
WETE |
PEMBA |
34.13 |
2 |
WILAYA YA NGORONGORO |
ARUSHA |
34.07 |
3 |
CHAKECHAKE |
PEMBA |
33.57 |
4 |
MJI WA NEWALA |
MTWARA |
27.22 |
5 |
MAGHARIBI |
UNGUJA |
26.48 |
6 |
WILAYA YA KALAMBO |
RUKWA |
26.32 |
7 |
KUSINI |
UNGUJA |
26.23 |
8 |
WILAYA YA BUKOBA |
KAGERA |
25.44 |
9 |
WILAYA YA MPIMBWE |
KATAVI |
24.43 |
10 |
WILAYA YA CHALINZE |
PWANI |
24.18 |
3.12
Halmashauri kumi (10) za mwisho.
Halmashauri kumi za mwisho zimepangwa kuanzia Halmashauri yenye ufaulu
mdogo kabisa kama zinavyoonyeshwa katika jedwali hapa chini.
3.13 Jedwali linaloonyesha Halmashauri kumi(10) za mwisho.
S/N |
JINA LA HALMASHAURI |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
WILAYA YA KILINDI |
TANGA |
9.09 |
2 |
WILAYA YA MADABA |
RUVUMA |
11.72 |
3 |
WILAYA YA BUHIGWE |
KIGOMA |
12.51 |
4 |
WILAYA YA KWIMBA |
MWANZA |
12.67 |
5 |
WILAYA YA NAMTUMBO |
RUVUMA |
12.71 |
6 |
WILAYA YA MKALAMA |
SINGIDA |
12.86 |
7 |
WILAYA YA MONDULI |
ARUSHA |
13.08 |
8 |
WILAYA YA NYANGH'WALE |
GEITA |
13.09 |
9 |
WILAYA YA NANYUMBU |
MTWARA |
13.33 |
10 |
WILAYA YA MAGU |
MWANZA |
13.55 |
3.14 Ufaulu kimkoa.
Mikoa imepangwa kuanzia
mkoa wenye ufaulu
wa juu kabisa hadi mkoa wenye ufaulu wa chini kabisa.
3.15 Jedwali linaloonesha
ufaulu kimikoa.
S/N |
MKOA/KISIWA |
WASTANI |
1 |
KISIWA CHA PEMBA |
33.85 |
2 |
KISIWA CHA UNGUJA |
24.25 |
3 |
DAR ES SALAAM |
21.95 |
4 |
KAGERA |
21.19 |
5 |
ARUSHA |
20.81 |
6 |
PWANI |
20.16 |
7 |
SONGWE |
19.85 |
8 |
RUKWA |
18.94 |
9 |
MOROGORO |
18.65 |
10 |
MTWARA |
18.47 |
11 |
LINDI |
18.34 |
12 |
MWANZA |
18.14 |
13 |
DODOMA |
17.97 |
14 |
TANGA |
17.8 |
15 |
IRINGA |
17.68 |
16 |
SHINYANGA |
17.52 |
17 |
GEITA |
16.88 |
18 |
KATAVI |
16.55 |
19 |
MANYARA |
16.55 |
20 |
KILIMANJARO |
16.49 |
21 |
KIGOMA |
16.38 |
22 |
MBEYA |
16.2 |
23 |
SINGIDA |
16.18 |
24 |
SIMIYU |
15.76 |
25 |
TABORA |
15.71 |
26 |
RUVUMA |
15.45 |
27 |
NJOMBE |
14.51 |
28 |
MARA |
14.3 |
|
18.4467 |
4. Tanbihi:
Matokeo kwa kila shule yanapatikana katika tovuti -www.iep.or.tz Imetolewa na Mwenyekiti
wa Islamic Education Panel Tarehe 23/08/2023.
MOHAMMED R. KASSIM MWENYEKITI IEP
TAIFA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni