NA MWANDISHI WETU
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza
kushughulikia changamoto za wazalishaji wa chumvi nchini kwa ajili ya kuongeza
uzalishaji wa chumvi nchini kuwa wa tija na manufaa.
Hayo amesema Meneja Uwezeshaji uchimbaji mdogo
Tuna Bandoma wakati wa Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji akizungumza
katika Kongamano la Wadau wa Chumvi lililofanyika Agosti 21, mkoani Lindi.
“Mikakati iliyopo ni mahususi kwa ajili ya
kuja na suluhisho ili kutatua changamoto zilizopo ambayo tumehusisha wadau,
tunakua na uelewa wa pamoja katika kushughulikia changamoto za wazalishaji wa
chumvi nchini, “ amesema Bando.
Aidha, amesema STAMICO inaendelea na hatua
mbalimbali ikiwemo hatua za haraka za kiwanda cha kusafisha chumvi katika
wilaya ya Kilwa na tayari Mkoa umeonesha eneo kwa ajili ya utekelezaji wa
kujenga kituo hicho.
Ameongeza kuwa, katika shamba darasa la
STAMICO wazalishaji wa chumvi watafundishwa namna mbalimbali ya kuyafikia
masoko kupitia ubora ili kuzalisha chumvi iliyo bora kufikia masoko ndani na
nje ili kuvutia wawekezaji
Mafunzo hayo ni moja ya utekelezaji wa kalenda
ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo inayofanywa na STAMICO.
Awali Kongamano hilo na mafunzo ya wazalishaji
chumvi lilifunguliwa na Mhe. Naibu Waziri wa Madini Dkt.Stephen Kiruswa Kwenye
Viwanja vya kilimahewa Wilaya Ruangwa Mkoani Lindi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni