Zinazobamba

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MBIO ZA HATUA YA FARAJA

Na Mussa Augustine.

Makamu  wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe amezindua rasmi ‘Kits’ za Maendeleo Bank Marathon ‘Hatua ya Faraja’ zitakazofanyika Septemba 2 mwaka huu huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 14, 2023 katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo  Dkt. Ibrahim Mwangalaba amesema kuwa  lengo la mbio hizo ni kuchangia fedha kwa ajili ya vituo viwili vyenye mahitaji maalum kwa watoto wenye usonji na watoto njiti.

“Karibu Maendeleo Bank Marathon 2023 "Hatua ya faraja" ina lengo la kuchangia shilingi milioni 200 kwa ajili ya vituo viwili  vyenye mahitaji maalum  Hospital ya Rufaa KCMC kwa ajili ya watoto  wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) na Kituo cha watoto wenye Usonji Mtoni Diakoni DSM,” amesema Dkt. Mwangalaba.

Dkt Mwangalaba amesema  kuwa kumekuwa na baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwaficha watoto wenye matatizo ya usonji hali ambayo inawafanya wakose haki zao za msingi ikiwemo elimu.

Amesemwa kuwa  watatumia mbio hizo kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwajali watoto Wenye usonji na kuwapatia haki na mahitaji yao kama watoto wengine.

Dkt. Mwangalaba ameeleza T-shirt za kukimbilia zitapatikana kwa kiasi cha shilingi 35,000 na kwamba mbio hizo zitajumuisha kilometa 21,10 na 2.5.

Halikadhalika amebainisha kuwa mbio hizo zitaenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa Damu ili kuweza kuokoa maisha ya wahitaji wa damu ikiwemowakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Hakuna maoni