Zinazobamba

Sakata la uwekezaji wa bandari Dsm… Waislam wamechagua kukaa kimya

 


Na Mwandishi wetu, Fullhabari Blog

Waislam wameuchukua waraka wa TEC wenye kurasa 8, wakautaza, wakausoma, wakauchambua kisha wakabaini kuwa huo ni mtego, wakachagua kukaa kimya. Hivi ndivyo unavyoweza kusema

Wanafahamu fika kuwa unapoanza kuandika tamko, inaonekana wazi kuwa unajibu hoja zilizowasilishwa na TEC, na mantiki hiyo TEC itakuwa imeshinda vita kirahisi sana, watatumia lugha tamu kuwa suala hili sasa limechukua sura ya kidini kwa hiyo ni vizuri zoezi la uwekezaji ukasitishwa kwa maslahi ya taifa.


Si wote wanaoweza kung’amua mtego huo, inahitaji akili kubwa, kwa mamntiki hiyo nawaona waislam hawatajisumbua kutoa matamko juu ya sakata hili la bandari wakiamini wazi kuwa serikali makini chini ya mama Samia Suluhu Hassan haiwezi kuwauza raia wake kama wapotoshaji wachache wanavyotangaza.

Hayo ni maneno ya mmoja wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye anachipukia kwa kasi sana Bw. Junaid Haithum wakati akipiga stori na Fullhabari Blog juu ya Tamko la TEC.

Haithum ameieleza Fullhabari Blog kuwa kwa vyovyote itakavyo anaona wazi kuwa waislam hawatakuja na tamko kuhusu bandari.

Haithum ambaye amekuwa mstari wa mbele kwenye kuyatazama mambo kwa mawanda mapana, amesema mtego ambao umetegwa na TEC ni kuwataka waislam kujibu andiko hilo na baadaye ionekane jambo hilo limeingia udini na hivyo kuhalalisha kusitishwa kwa uwekezaji katika bandari

“Ukiniuliza kama waislam wanahaja ya kuja na tamko nitakwambia hapa, ni bora wakae kimya kwa sababu hesabu za TEC ni kuwachokoza waislam ili wajibu hoja na hapo ndipo watakuja na hoja kuwa zoezi la uwekezaji katika bandari inapaswa kuachwa.

Hivi karibuni TEC ilikuja na tamko la kutokuunga mkono uwekezaji wa bandari, hata hivyo wengi wamekosoa andiko hilo wakisema limekuwa general, badara ya kushauri nini kifanyike katika vifungu lakini wao wameukataa uwekezaji wote. Haikufahamika mara moja kama chanzo cha kukataa uwekezaji huo ni kwa sababu muwekezaji anatoka taifa la waraabu au kitu gani.

Ends,


Hakuna maoni