Zinazobamba

TANZANIA ,MALAWI KUSHIRIKIANA UZALISHAJI WA UMEME MTO SONGWE.

 


Dar es salaam,

Na Mussa Augustine.

SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya nishati ya umeme kati ya Tanzania na Malawi ili kuhakikisha nchi hizo zinakua na upatikanaji wa nishati ya Uhakika.

Akizungumza leo Agosti 10, 2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kusaini Makubaliano ya Ushirikiano huo, Waziri wa Nishati, Mh. January Makamba, amesema kwamba Makubaliano hayo yanahusu Ushirikiano kwenye maeneo ya uzalishaji wa umeme wa maji kupitia Mto Sogwe ambao upo pande mbili ambazo ni Tanzania na Malawi.

Waziri Makamba amebainisha kuwa mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 300 ,nakwamba unakwenda kusaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo uwekezaji wa viwanda Nchini.

Aidha Waziri huyo wa Nishati ameendelea kusema kuwa ushirikiano huo unakwenda kupanua wigo mkubwa katika uzalishaji wa Umeme ikiwemo kufanya utafutaji wa gesi pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Umeme kwa nchi hizo.

"Ili tuweze kufanikiwa katika utekelezaji wa makubaliano haya,tumekubaliana kuweka kamati ya wataalamu kutoka pande zote mbili ili kuweza kufatiliana kwa pamoja utekelezaji wake"Amesema Waziri Makamba. 

Nae Waziri wa Nishati nchini Malawi Mh.Ibrahim Matola, amesisitiza kuwa ushirikiano huo unakwenda kuleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi huo wa uzalishaji wa Umeme.

Waziri Matola ameongeza kuwa makubaliano hayo ni muhimu kutokana nakwamba uzalishaji wa umeme katika Mto Songwe unakwenda kuleta maendeleo ya kiuchumi baina ya Tanzania na Malawi kwani utachochea uwekezaji.

" Mradi huu pamoja na mambo mengine utasaidia kuongeza megawti za umeme katika gridi ya taifa kwa nchi hizi mbili hivyo utasaidia kuwa na uwekezaji wa uhakika katika miradi mbalimbali ya kiuchumi." Amesema Waziri huyo wa Nishati wa Malawi.


Hakuna maoni