Zinazobamba

JUMUIYA YA KIISLAM TANZANIA YAIOMBA SERIKALI IENDELEE KUANDAA MITAALA YA DINI NA VITABU VYA KUFUNDISHIA


Na Mussa Augustine

JUMUIYA  ya Kiislamu Tanzania imeomba Serikali  kuendelea kuandaa mtaala ya Dini na Vitabu vya kufundishia.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam Alhajj Shelk Mussa Kundecha amesema Jumuhiya na taasisi za kiislamu nchini imepokea kwa masikitiko makubwa kwa Serikali kuja namfumo mpya wa masomo ya Dini.

 "Kwamfano kwenye Serikali kuna Pombe halali na Pombe haramu wakati katika Uislamu pombe zote ni Haramu".Alisema Sheikh Mussa kundecha.

 Shelkh kundecha alisema kuwa serikali haitakiwi kuipangia mitaala ya masomo ya Dini,Badala yake waziache taasisi za kiislamu kutengeza mitaala yao wenyewe.

Aidha amesema kuwa somo la Dini haliwezi kuratibiwa na Serikali,hivyo waaziache taasisi za dini ziratibu mitaala yake zenyewe.

Hakuna maoni