MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI JAJI FRANCIS MUTUNGI AWATAKA WANASIASA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi
Na Mussa Augustine
Msajili wa
Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi ametoa wito kwa vyama vya siasa kufanya
siasa zenye ustaarabu na zinazozingatia Sheria ili kuendelea kulinda Amani ,Utulivu
pamoja na Umoja.
Hayo
ameyasema Agost mosi ,2023 wakati wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa
lililowakutanisha viongozi wa dini na vyama vya siasa likiwa na malengo ya
kuelimishana namna ya kufanya siasa safi zitakazolinda utu na Taifa kwa ujumla.
Aidha amesema
kwamba Baraza la Vyama vya siasa limekua likifuatilia mwenendo wa siasa
zinazoendelea hapa nchini,nakwamba limeona liwakutanishe viongozi wa kisisasa
pamoja na viongozi wa dini ili
kuelimishina jinsi ya kufanya siasa kwa kuzingatia mipaka ya kazi za siasa na dini.
"Leo tumekutana
na viongozi wa dini na viongozi wa siasa
kwani tumekua tukifuatilia siasa zinazoendelea hapa nchini tumeona sio nzuri
kwani kumekuwa na matumizi lugha za
matusi na kukejeli,pia viongozi wa dini kuhusishwa kwenye siasa hizo."
amesema Msajili huyo wa Vyama vya Siasa Nchini.
Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Alexander Makulilo amesema kuwa uhusiano wa siasa na dini ni changamano hivyo serikali inapaswa kuweka Sheria ili kudhibiti Muungano huo, nakwamba sheria zimekataza kutumia viongozi wa dini katika Majukwaa ya Siasa wakati wa kunadi sera za vyama vyama vya siasa..
Makulilo
amesisitiza kuwa Matumizi ya lugha za uchochezi, kudharirisha nchi, lugha za kibaguzi,
lugha za udharirishaji wa jinsia zimepigwa marufuku badala yake vyama vya siasa vinapaswa kuuza
sera zao ili waungwe mkono.
Aidha
ameendlea kusema kuwa Sheria hairuhusu
chama chochote Cha siasa kuwa na walinzi wa viongozi na Mali za chama badala
yake kazi hiyo ni ya jeshi la polisi.
Kwa upande
wake mwanasiasa Mkongwe John Cheyo amewaomba wanasiasa nchini kuwa wazalendo
kwa nchi yao kwa kufanya siasa zisizodhalilisha nchi wala kumtukana Rais na kiongozi yeyote wa
serikali na chama,nakwamba waendelee kudumisha tunu za Taifa ambazo ni
Umoja,Amani na Mshikamano.
"Ni aibu kwa kiongozi wa siasa kusimama jukwaani na kuanza kuisema nchini yako na viongozi wako hiyo sio siasa ambayo inapaswa kuwepo huo sio uzalendo, tunapaswa kuwa wazalendo kwanza kwa nchi yetu." amesema mwenyekiti huyo Taifa wa UDP Jonh Cheyo
Naye Padri Frolence Lutaiwa kutoka Baraza la maaskofu (TEC) amesema viongozi wa dini wanapaswa kukemea maovu na si kushiriki katika uovu hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuwaasa wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu zenye kujenga umoja, amani na mshikamano wa Taifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya na Taasisi za kiislam nchini shekh Musa Kundecha amesema ni ngumu kutenganisha dini na siasa hivyo viongozi wanapaswa kutumia majukwaa ya siasa kutangaza amani na imani ili kufanya wananchi kuwa na hofu ya Mungu na si kuwabagua kutokana na uchama au udini.
Hata hivyo baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Democrat Party (DP) Abdul Mluya wamesema kuwa mkutano huo umewasaidia kuwakumbusha mambo mengi nakwamba yale yote waliyoelekezwa watayazingatia katika kudumisha Amani na Utulivu kwa Taifa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni