TABIBU MADUHU AIHIMIZA JAMII KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI KWA AJILI YA KUEPUKANA NA CHANGAMOTO ZA KIAFYA
Na Mussa Augustine
Jamii
imeendelea kukumbushwa kutumia vyakula vya asili Ili kuweza kuepukana na
changamoto mbalimbali za kiafya ikiwe afya ya uzazi.
Rai hiyo
imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa kituo Cha Utafiti na
tiba asilia cha NYASOSI tabibu Emmanuel Maduhu wakati akizungumza na Vyombo vya
habari ofisini kwake Magomeni jijini humo.
Tabibu Maduhu
amesema kuwa tatizo la uzazi kwa
wanandoa wengi limekua kubwa hali ambayo imekua ikisababisha familia na ndoa
nyingi kuvunjika kutokana na wanandoa hao kukosa watoto ,hivyo sababu hiyo
imekuwa ikichangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo mfumo mbaya wa ulaji wa vyakula
vya viwandani.
"
Matatizo ya Uzazi ni changamoto kubwa kwa kizazi Cha Sasa,ndoa na familia
hazina amani kwasababu ya kukosa watoto ndani ya familia,na hili tatizo
linapotokea mwanamke ndio anaelaumiwa huku Kumbe ni tatizo la wanandoa wote
,ambapo wanatakiwa kuwaona wataalamu wa afya ili waweze kupatiwa matibabu
" amesema tabibu Maduhu.
Nakuongeza
kuwa mwanaume anaweza kua anashiriki vizuri tendo la ndoa lakini kumbe mbegu
zake za kiume hazina uwezo wa kutungisha mimba ,hivyo wanatakiwa waendesha
wakapate vipimo Ili kujua tatizo lipo kwa nani na kuanza kupata matibabu Ili
wapate mtoto inawezekana kabisa" amesisitiza.
Amesema kuwa
baadhi ya chanzo Cha matatizo ya Uzazi ni pamoja na matumizi mabaya ya taulo za
kike( Pads) ambapo zimekua na bakteria wanaochangia matatizo ya Uzazi,kutumia
kwa wingi vyakula vya viwandani,pamoja na matumizi mabaya ya dawa, hivyo
wananchi wanapaswa kujiepusha na hali hiyo .
"
Twende edeni tutumie vyakula vya asili, ambapo vingine tunauwezo wa kuvilima
sisi wenyewe,kwahiyo ukianza kuona dalili za kupata maumivi ya tumbo chini ya
kitovu,au maumivu ya tumbo na mgongo unapaswa kwenda kumuona daktari upatiwe
vipimo ili kujua kama ni tatizo la uzazi na unaweza kuja kwenye kituo chetu cha
NYASOSI ili upate matibabu upone kabisa na uweze kupata mtoto bila shida yoyote" amesema
Katika hatua
nyingine tabibu huyo amesema kuwa Wanaume wengi wamekua wakisumbuliwa na ugonjwa wa
tezi dume kuazia umri wa miaka 40 na kiendelea kutokana na kiungo ambacho kipo
chini ya kibofu cha mkojo kupata uvimbe hivyo hali hiyo imekuwa ikiwasumbua
Wanaume wengi bila kua na uelimu ya kutosha.
Amesema kuwa
tezi dume hiyo inakua inatanuka kulingana na umri wa mwanaume nakwambia endapo
ikipata jeraha wakati wa kutanuka ndipo inaposababisha matatizo kutokea ikiwemo
kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku kutokana na mshipa wa kibofu kubanwa
inaweza kusababisha pia saratani ya kibofu Cha mkojo.
"Mwanaume
ukianza kuona dalili ya tumbo kujaa gesi na kuunguruma,au kupungua kwa nguvu za
kufanya tendo la ndoa,unatakiwa kuangalia wataalamu hivyo zingatia sana hizi
dalili Ili usikae muda mrefu mpaka tatizo liwe kubwa" amesema Tabibu
Maduhu.
" Nakuongeza sisi hapa tuna dawa zilizothibitishwa na serikali,tuna dawa inaitwa Ntundwa ambayo inatibu tezi dume kwa muda wa siku Saba tu unapona kabisa,hivyo wale wenye matatizo ya ugonjwa huu wafike hapa ofisini kwetu au watutafute kwa mawasiliano yetu 0788330105 tunaweza kuwapatia mahali popote walipo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni