GLOBAL EDUCATION LINK KUENDELEA KUTATUA CHANGAMO ZA UPATIKANAJI WA NAFASI ZA MASOMO KATIKA VYUO VIKUU
Na Mussa Augustine.
Kampuni ya Uwakala wa Kimataifa wa kushauri na kudahili Wanafunzi kwa ajili ya kusoma Elimu ya Juu Nje ya Nchi ya Globala Education Link imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nafasi za masomo katika Vyuo Vikuu ndani na nje ya nchi.
Hayo
yamesemwa leo Julai 22,2013 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Abdulmalik Mollel wakati
akizungumza na Waandsishi wa habari baada ya kuhitimishwa kwa Maonyesho ya 18
ya Elumu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kuanzia Julai 17 mwaka
huu chi ya Tume ya Vyuo Vikuu Nchini(TCU)
Aidha Mollel amesema kuwa tangu Maonyesho hayo yaanze yamekuwa na mwitikio Mkubwa ambapo
wamefanikiwa kufanya udahili kwa wanafunzi wengi ukilinganisha na maonyesho ya
miaka iliyopita.
Aidha
amebainisha kuwa pamoja na kuhitimishwa kwa maonyesho hayo katika viweanja vya
Mnazi Mmoja lakini Kampuni ya Global Education Link itaendlea kufanya udahili
kwa wanafuzni ambao wameshindwa kufika katika viwanja vya mnazi mmoja.
“Sisi kama Global Education Link tutaendlea na udahili katika ofisi zetu zilizobo barabara ya Nyerere ,hivyo wale wote ambao hawakufanikiwa kufika katika maonyesho ya Mnazi Mmoja wanaweza kufika pale ofisini nakupata huduma kuanzia jumatatu ya tarehe 24 mwaka huu”Amesema Mollel
Nakuongeza
kuwa udahili huu utaendelea hadi tarehe nane siku ya nane,lengo letu ni
kusaidia wale ambao hawajapata udahili wa Masomo ya Elimu ya Juu katika Vyuo
vikuu vya ndani na nje ya Nchi.
Katika hatua
Nyingine Abdulmalik amesema kuwa Kampuni yake imefanikiwa kufanya udahili wa
wanafunzi wapatao 43 wa kitazania ambao hawakufanikiwa kumaliza masomo nchini
Sudani kutokana na Machafuko ya Vita yanayoendelea.
“Hawa wanafunzi wamepata katika vyuo Vikuu Vya Nje ikiwemo India,Uturuki,Cyprus ,Malaysia hivyo ni jambo zuri ambalo limetupa faraja kuona tumewasaidia wanavyuo hawa wengine walikua mwaka wa 2 na mwaka wa 3 chini Sudani,waweze kumaliza masomo yao”amesema Mollel
Pia
ameongeza kuwa Wanafunzi wapatao 193 ambao
ni raia wa Sudani wamejiandikisha ili wafanyiwe udahili wa nafasi za masomo
katika Vyuo Vikuu ndani na nje ya Nchi tunavyoshirikiana navyo ,hali ambayo ni
mafanikio makubwa tuliyoyapata .
Hakuna maoni
Chapisha Maoni