Na Mussa Augustine.
Wanafunzi waliokwama
kimasomo Nchini Sudan kutokana na machafuko na vita vinavyoendelea nchini
humo,wametakiwa kuitumia Global Education Link kuwaunganisha na Vyuo Vikuu
vingine ndani na Nje ya Nchi ili wasipoteze Muda muda mwingi kusubiria
kumalizika kwa machafuko hayo na hata kupoteza dira ya masomo yao.
Wito huo umetolewa Julai
18 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link Abdulmalik Mollel
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda lao lililopo kwenye
maonyesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yanayoandaliwa na Tume ya
Vyuo Vikuu Nchini (TCU) Ambayo yanaendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jiji
Dar es ambayo yameanza July 17 na kutarajiwa kutamatika July 22 mwaka huu 2023.
Abdulmalik Amesema
upatikanaji wa Chuo Kikuu Bora Cha kujiunga kuendelea na mwaka wa masomo katika
ya Muhula ama kuendelea na mwaka wapili au zaidi ni changamoto Duniani kote.
"Tumeona hivi
karibuni Vijana wetu wa kitanzania wamekwama katika vita na inawezekana kati
yao bado wapo Tanzania,na inawezekana bado hawajabahatika kupata Vyuo Vikuu vya
kuhamia,unajua Kujiunga na Chuo Kikuu sio tatizo ila kupata Chuo
kinachokuruhusu wewe Mwanafunzi ma mwaka wa pili kwenda watatu ili usipoteze
kile ulichokuwa umeanza kukisoma,upatikanaji Wa Vyuo Vikuu hivyo Duniani kote
huwa ni tatizo"
"Mwanafunzi huyo
aliyekwama asiamini amekwama, Vyuo Vikuu Vya Ndani vyenye uwezo wa kuwachukua
viwachukue,na Vyuo Vikuu vya Nje ninawahakikishia njooni kwenye maonyesho haya
ya TCU ndiko platform pekee,Usiendelee kupoteza miaka yako minne ama Miwili au
mitatu ya udaktari, engineering,Ama biashara ama ni Kozi yoyote ile uliyokuwa
Sudan,alafu hujui sudani vita itaisha lini"
"Maadamu Taasisi
ya Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi Global link ipo katika maonyesho haya wewe
mwanafunzi ambaye umetoka huko upo,inawezekana ukawa huna matokeo yako yote
kwasababu kwenye vita kuna shida,inawezekana vyeti vyako umeviacha huko Sudan
sasa anayeweza kukuelewa kirahisi ni mimi Mtanzania ndie ninaweza nikajua
nifanye nini ili nihakikishe unapata chuo kingine".
Aidha amebainisha kuwa
Wanafunzi wote watakao fika kwenye maonyesho hayo na kutembelea Banda la Global
Education Link Wataweza kuunganishwa kwa haraka na Vyuo Vikuu vingine vya Nje
na kwa gharama ileile ya Chuo walichotoka.
"Mkikanyaga
katika maonyesho haya kwenye Banda la Global Education Link mwanafunzi
uliyotoka uliyekwama umetoka Sudan na unatamani kuunga Elimu yako Nje ya Nchi
na kwa gharama ileile wewe njoo kuanzia kesho nielezee nikithibitisha umekidhi
vigezo vya kusoma Chuo Kikuu ni jukumu langu pamoja na wewe kuwasiliana nachuo
chako cha Sudan kwasababu wanawasiliana sio kwamba hawawasiliani tutapa
recommendation latter na wakishindwa kutupatia tutaweka Guarantee kama Global
Education Link kwa partners wetu ili kuhakikisha mtanzania hawezi kupoteza Elimu
yake"
Pia amewahakikisha
wale wote watakaofika Global Link kuhudumiwa na kupatiwa Chuo Kikuu
wanachokihitaji ndani ya Masaa 72 pekee na kwawale wenye changamoto ya kifedha
wafike watapatiwa mikopo isiyokuwa na riba kutoka katika Benki washirika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni